Uongozi wa vyama vya siasa vikuu viwili vinavyounda Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Chama cha Mapinduzu(CCM) pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) kwa pamoja wamekubaliana kugawana madaraka ya nafasi ya makamu mwenyekiti.
Nafasi hiyo ambayo kwa vipindi vinne vilivyopita ilikuwa ikiongozwa na madiwani kutoka chama cha wananchi- CUF sasa itaongozwa na diwani kutoka Chama cha mapinduzi CCM,
Makubaliana hayo yamefikiwa baada ya mvutano wa siku nzima jambo lililopelekea wajumbe wa pande zote mbili kukutana ili kufikia muafaka baada ya idadi ya wajumbe kila upande wajumbe 17.
Baada ya wajumbe kurudi kwenye kikao mnamo SAA 12 jioni mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Abuu Musa alisoma makubaliano ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili kisha wawakilishi kutoka kila upande walisaini hati ya makubaliano hayo.
Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kamati ambapo;
#Kamati ya fedha itaongozwa na Mwenyekiti(CUF)
#Kamati ya Ukimwi itaongozwa na CCM,
#Kamati ya Mazingira itaongozwa na CUF na
#Kamati ya Elimu ,Afya na huduma za jamii ikiongozwa na CCM.
Baada ya makubaliano ya kutiliana saini mwenyekiti aliahirisha kikao mpaka kesho tarehe 13/9 ambapo wataendelea na ajenda zingine.