**********************
Kuelekea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu wasimamizi wateule kutoka wilaya ya Biharamulo,Muleba,Missenyi,Karagwe,Kyerwa,Ngara,Bukoba DC,Bukoba MC, mkoa wa kagera wameapishwa leo mkoani humo.
Nae mwanasheria Adivocet Jovin Rutainulwa ametoa maelezo kuhusu kiapo walicho Hapa wateule hao huku akisisitiza kanuni za uchaguzi kuwa kufuatwa na kuzingatiwaa na wateule hao.
“kanuni ya 44 ya tanagazo la serikali namba 371 ya mwaka 2019 na kanuni ya 47 ya tangazo la serikali 372 ya mwaka 2019 kanuni hizi zote nilizozitaja kwa pamoja ndizo zinazo simamia uchaguzi wa serikali za mitaa pia kiahapo hicho watakachokula kipo kwa mjibu wa sheria pia kipo kwa mjibu wa sheria ya viapo na matamko ya kisheria sura ya 34 kama ilivyo tungwa na bunge na wanawajibika kukilinda kiapo hiki na kama wakikkiepuka watakuwa wametenda kosa la kijinai na watashitakiwa kwa kosa la kijinai”Alisema Adivocate Jovin Rutainulwa.
Uapisho huo ulioshuhudiwa na katibu tawala wa mkoa kagera Prof.Faustini Kamzola,Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi mkoa Mh.Rubanzibwa Projectus,pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya mkoa huku wateule hao kutoka wilaya zote nane za mkoa wa kagera wakisaini makubaliano ya kusimamimia na kuwajibika vizri katika usimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo katibu tawala wa mkoa wa kagera Prof. Faustin Kamzola ametaja watu wanaotarajiwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ni wananchi Milon 1,288,570 wanaotarajiwa kujiandikisha na vituo vya kujiandikisha ni elf 3738 vitongoji 3665 vijiji 662 ambavyo vinatokana ka kata 192 na tarafa 27 katika mkoa wa kagera.
Sambamaba na hayo mmoja wa wateule wa usimamizi wa uchaguzi huo kutoka wilaya ya Muleba Bi. Essery Felician Pima ambae pia ni Afisa utumishi wa Wilaya ya Muleba amewasisitiz wananchi kujitokeza katika kujiandikisha kupiga kula.
“Kimsingi nawasisistiza wananchi kutoka katika Wilaya ya Muleba kwamba haki itatendeka sheria itazingatiwa utaratibu na miongozo itafuatwa katika kuhuakikisha kwamba taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa niwaombe tu wananchi kujitokeza kwa wingi maana tunaamini katika kupiga kura pia watakuwa ni wengi”Alisema Bi. Essery Felician.
Vile vile Bi. Essery Felician Pima ambae pia ni Afisa utumishi wa Wilaya ameyataja makisio au mataraji katika Wilaya yake ya Muleba kwa wananchi wanatarajiwa kujiandikisha ni Laki 323055 kutoka kata 43 vijiji 166 na vitongoji 752.