Waziri wa Maji Mhe.Prof.Makame Mbalawa ,akiwahutubia wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,akitoa taarifa kwa wananchi wa Kata ya Nghong’onha iliyopo Mkoani Dodoma Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na Ajira,Mhe.Anthony Mavunde,akiwaelezea wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi,akizungumza na wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma wakifatilia hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Katika kata hiyo .
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akifungua kitambaa akiwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,tayari kwa ajili ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma kulia ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akipeana mkono na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,mara baada ya kumaliza kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma kulia ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi.
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,aakiwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,wakifungua maji kwenye kisima mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,pamoja na Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,wakimtwisha maji mwanamama wa kata ya Nghong’onho baada ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma .
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na Ajira,Mhe.Anthony Mavunde,akimtwisha ndoo ya maji wananchi wa Kata ya Nghong’onha jijini Dodoma baada ya kuzinduliwa Mradi wa Maji Katika kata hiyo
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akimtwisha ndoo ya maji mwananchi wa kata ya Nghong’onho baada ya kuzindua Mradi wa Maji katika Kata hiyo
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akimtwisha ndoo ya maji Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl,baada ya kzuindua Mradi wa Maji katika Kata ya Nghong’onha iliyopo mkoani Dodoma .
Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa,akiwa picha ya pamoja viongozi wa GIZ.
…………………
Na.Alex Sonna,Nghong’onha,Dodoma
SERIKALI imesema kuwa imejipanga kukarabati miradi yote ya maji iliyotelekezwa kwa kipindi kirefu ili kupunguza adha ya uhaba wa maji kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbalawa wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Nghong’onha Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji Katika kata hiyo .
Waziri Mbalawa amesema makandarasi wa ovyo wamekuwa wakikwamisha juhudi za serikali Katika maendeleo na kusababisha hasara hivyo kuwataka kujitathimini upya.
“Serikali haitomfumbia macho mkandarasi yeyote anayegeuza miradi ya maji Kama kitega uchumi chake,lazima kila mtu akae kwenye mstari kuhakikisha anafanya maendeleo kwa moyo mmoja,”amesema.
WaziriProf.Mbalawa amesema Mradi wa maji Katika kata hiyo ulianza tangu mwaka 2013 ambapo umechukua miaka 7 kukamilika kwake huku akilipongeza Shirika la Maendeleo la Ujeruman [ GIZ ]Kwa kufanikisha mradi huo.
“Huu ni uzembe mkubwa ,Mradi wa maji unachukua miaka mingi tunaweza kuufananisha na umri wa mtoto ambapo mwaka 2013 angezaliwa mwaka angeanza darasa la kwanza,”alisema na kuongeza,
“Katika Mradi huu kulifanyika uzembe wa hali ya juu na uhuni kwani Mradi huu ulitakiwa kukamilika kwa kipindi Cha miezi sita tu tangu kuanza kwake,”alisisitiza Mbalawa.
Kutokana na hayo amewataka watendaji wote wa wizara ya maji kuhakikisha wanakuwa makini kushughulikia miradi ya huduma za kijamii ili kuhakikisha inaondoa kero kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Wizara ya Maendeleo ya Uchumi na Ushirikiano wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bi Vera Rosendahl amesema kukamilika kwa mradi huo ni mafanikio makubwa ya uhusiano wa Tanzania na Ujerumani.
Mradi huo utasaidia zaidi ya watu 12,000 ambao hawakua na uwezo wa kupata maji safi na hivyo sasa suala la ukosefu wa maji Nghong’onha . linaenda kuwa historia.
” Kwa kufahamu umuhimu wa maji kwa wananchi na kumtua mama ndoo sisi tulitoa kiasi cha Shilingi Milioni 350 ili kuwezesha kukamilika kwa mradi huu.
Tunawashukuru sana Wizara ya Maji, Halmashauri ya Jiji la Dodoma na zaidi wananchi wa eneo hili kwa namna ambavyo wametoa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha mradi huu,” Amesema Bi Rose.
Ameahidi kuendeleza ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi hasa katika miradi ambayo inayagusa maisha yao moja kwa moja.
Naye mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (DUWASA)Mhandisi David Palangyo aliishukuru serikali ya Ujerumani kujitolea kushirikiana nao kutatua kero ya maji kwa wakazi wa Kata ya Nghong’onha .
Mhandisi huyo amesema wao Kama wadau wa maji watahakikisha wanakuwa karibu na wakazi hao kuhakikisha wanalinda miundombinu ya maji huku wakijipanga kuanzisha kamati ya maji ya kata hiyo itakayosimamia mapato kwa uzalendo.
“Hakuna asiyefahamu shida nliokuwa mkiipata,na Sasa mmepata maji moiyoyatamani kwa kipindi kirefu tafadhalini ndugu zangu tushirikiane kwa pamoja kuyaenzi kwani maji ni uhai,”alisema.
Pia amefafanua kuwa kabla ya Mradi huo kukamilika wananchi walikuwa wakitumia maji yasiyo salama na kwamba walinunua ndoo moja ya maji kwa shilingi miatano ambapo kwa Sasa Lita 20 ya maji itauzwa kwa shilingi 25.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ,ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Patrobas Katambi aliwataka wananchi wa Nghong’onha kuitunza miundombinu ya maji na kuepuka kuihujumu.
“Tunafahamu Kuna watu hawapendi maendeleo nataka kuwaambia kila mtu awe mlinzi wa mwenzie ,hakikisheni pia mnalinda mazingira ya vyanzo vya maji ili kiendelea kufurahia huduma hiyo,”amesema.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi ,vijana na Ajira,Mhe.Anthony Mavunde amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambapo amebainisha kuwa alikuwa halali usiku na mchana kutafuta mwarobaini wa kutatua kero ya maji.
“Wakati nasaka kura hapa nilisema yasipokuja maji Nghong’ona mpaka kufikia mwaka 2020 msinipigie kura,Moyo wangu ulikuwa unadunda sasa inakaribia 2020 na Maji bado,nililuwa silali napita hapa na pale kuhakikisha tatizo la uhaba wa maji linatatuliwa,lakini sasa imekuwa historia tujivunie tatizo hili ni la muda mrefu .amesema.
Kwa upande wao Baadhi ya Wananchi wa kata hiyo wamesema uzinduzi wa Mradi huo wa maji utawasaidia kuepukana na kero kubwa ya adha ya maji ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ambapo awali ndoo moja walikuwa wananunua kwa Tsh.300 hadi 400 lakini sasa watakuwa wananunua kwa Tsh.25 tu kwa ndoo katika mradi huo hali ambayo itapunguza ukali wa Maisha.
Jumla ya wakazi 10500 wa Kata ya Nghong’onha wanatarajiwa kunufaika na Mradi huo.