Home Uncategorized 2173 Waanza mitihani ya darasa la Saba halmashauri ya wilaya ya Njombe

2173 Waanza mitihani ya darasa la Saba halmashauri ya wilaya ya Njombe

0
Jumla ya wanafunzi 2173 wa darasa la saba  wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Katika mtihani huu unaotarajia  kufanyika kote nchini kuanzia septemba 11 hadi 12  jumla ya wavulana 948 na wasichana 1225 wanatarajia kufanya mtihani huu kutoka katika shule 52 za serikali kati ya shule 55 za msingi zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
wanafunzi ambao wanafanya mtihani huu ni wale walioingia darasa la kwanza mwaka 2013 ambapo jumla ya wanafunzi 2,659 waliandikishwa, wavulana wakiwa 1225 na wasichana 1434.
Tayari maandalizi yote muhimu kwa ajili ya ufanyikaji wa mitihani huo ikiwemo upelekeji wa mitihani katika vituo teule vya kuhifadhia mitihani yameshafanyika.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inapenda kutoa wito kwa wazazi, na walezi wa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani kuhakikisha wanawapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowawezesha kufanya mtihani katika hali ya utulivu.
Wito unatolewa  kwa wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi  kutojiusisha na mbinu zozote zile za udanganyifu wakati wa kufanya mtihani ambazo zitapelekea kufutiwa matokeo yao.
Sambamba na hilo wasimamizi wa mitihani wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia  kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mitihani pamoja na utumishi wa umma  ila kuhakikisha mitihani inafanyika na kumalizika bila dosari yoyote.
Katika mtihani uliofanyika Mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 2278  kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wavulana walikuwa 1032 na wasichana 1246 huku kiwango cha ufaulu kikiwa ni asilimia 74.65
Aidha, kwa mwaka 2019 Halmashauri ya wilaya ya Njombe inatarajia kufaulisha kwa zaidi ya asilimia 80