Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi wakati wahafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na ofisi yake.
Katibu Mkuu Msaafu wacOfisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akieleza historia yake katika utumishi wa umma (Miaka 34) kwa timu ya menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) hiyo Bi. Maimuna akizungumza na timu ya Menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga kwa kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria za utumishi.
Mhasibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Anthony Chayeka akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
********************************
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi kwa utendaji wenye weledi kwa kipindi cha miaka 34 alichotumikia katika utumishi wa umma.
Ametoa pongezi hizo wakati wa hafla fupi ya kumuaga na kumpongeza katibu mkuu huyo aliyestaafu utumishi wake wa umma kwa mujibu wa sheria za utumishi nchini mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba Jijini Dodoma.
“Kwa dhati nachukua nafasi hii kumpongeza Bi. Tarishi kwa namna alivyotumikia Taifa hususani akiwa katika Ofisi hii ya Waziri Mkuu, amefanya vizuri na alijitahidi sana kusimamia vyema ofisi kuhakikisha ofisi inaenda vizuri na hakika unastahiri pongezi kwa kuzingatia ulivyotekeleza majukumu yako kwa busara na weledi wa hali juu,”
Waziri aliongezea kuwa, mchango wa Katibu mkuu huyo ni mkubwa kwa kuzingatia namna alivyotumika kwa miaka mitatu katika ofisi hiyo kwa kuhudumia Ofisi binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu pamoja na Uratibu wa Shughuli zote za Bunge.
“Umekuwa ni kiungo muhimu katika kuhakikisha shughuli za Mhe.Waziri Mkuu pamoja na bunge zinatekelezwa katika viwango vya hali ya juu kwa kusimamia vyema hivyo tutakumbuka mchango wako kwa kipindi chote ulichokuwa nasi,”alisema Waziri Mhagama
Aidha Waziri alipongeza timu ya menejimenti ya ofisi hiyo na kukiri kuridhishwa na utendaji wao wenye ufanisi na weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi, kanuni na sheria za utumishi wa umma.
“Kipekee ninawapongeza timu ya menejimenti kwa usimamizi wenu mzuri wa ofisi hii hivyo niwatie moyo muendelee kutekeleza majukumu yenu ili kuzaa matunda yanayoonekana kwa kuzingatia ofisi hii ni mratibu wa shughuli zote za serikali,”Alisisitiza Waziri Mhagama
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi alishukuru Ofisi ya Waziri mkuu kwa namna walivyochangia katika utekelezaji wake wa majukumu kwa muda aliotumikia katika ofisi hiyo toka tarehe 4 Aprili 2017 alipoteuliwa kusimamia shughuli za Bunge na Waziri Mkuu.
Aidha Tarishi aliiasa timu ya menejimenti kuendelea kuwatumia watumishi vijana katika kutekeleza majukumu kwa kuzingatia uwezo waliona katika kufiri, kutenda na kujituma kwa dhati.
“Nishauri Watendaji mnaobaki wekezeni kwa vijana kwa kuzingatia wanauwezo mkubwa wa kufikiri kwa haraka, wepesi kutenda na wakiaminiwa wanatekeleza kwa juhudi ili kuthibitisha uwezo wao hivyo muwatumie kwa tija na maendeleo ya nchi yetu’”alisema Tarishi
Aidha aliongezea kuwa, uwepo wa vijana katika ofisi za umma unamchango mkubwa kwa kuzingatia uwezo walionao wa kubuni mbinu mbalimbali zinazorahisisha utendaji kazi kwa kuzingatia ukuaji wa sayansi na teknolojia hivyo wekezeni nguvu kwa kundi hilo.
“Chukue fursa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia katika kuboresha ufanishi na ubunifu katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku kwa kuwekeza kwa vijana, kwa kuwatia moyo na kuwaelekeza pindi inapobidi ili kuleta matokeo chanya katika kutekeleza majukumu ya kila siku,”alisisitiza Tarishi.