Home Mchanganyiko WANAFUNZI WA SHULE YA ATLAS WAASWA KUJIANDA VYEMA KWA MITIHANI IJAYO

WANAFUNZI WA SHULE YA ATLAS WAASWA KUJIANDA VYEMA KWA MITIHANI IJAYO

0

Mkuu wa Shule ya Sekondari Atlas Grace Nalubega akizungumza na wazazi na wanafunzi wakati wa maombi rasmi ya kuwaombea wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kidato cha nne.

**************

Na JUMA ISSIHAKA

WANAFUNZI wanaotarajia kufanya mitihani ya kumaliza darasa la saba na Kidato cha nne mwaka huu, wametakiwa kujiandaa kuepukana na matumizi ya nyenzo zozote za udanganyifu katika vyumba vya mitihani.

Kauli hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa matukio ya udanganyifu katika vyumba vya mitihani katika shule mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa maombi rasmi ya kuwaombea wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani hiyo, yaliyofanyika katika shule ya Sekondari na Msingi Atlas jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Shule ya Sekondari Atlas Sara Nalubega, alisema iko haja ya wanafunzi kujiandaa vyema ili kuepuka udanganyifu.

Alisema sababu za kutokea kwa matukio hayo katika shule nyingi nchini ni kutokana na wanafunzi wengi kutokuwa na maandalizi ya kutosha hivyo kujikuta wakitafuta namna rahisi ya kufaulu mitihani.

Akizungumza kuhusu shule hiyo Sara, alisema wanafunzi wake wamekuwa wakifanya vizuri katika mitihani hiyo, kutokana na kuwa na maandalizi ya kutosha na kumtanguliza mungu kabla ya kufanya mitihani.

“Kila mwaka tumekuwa na utaratibu wa kufanya maombi kuelekea mitihani, pia hata tukimaliza tunashukuru huu ndiyo utaratibu wetu wa kila mwaka, “alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Atlas Ubungo jijini Dar es Salaam
Justus Kagya, alisema ni vyema watoto hao wakatulia katika vyumba vya mitihani na kuhakikisha wanajibu maswali kama vile walivyoulizwa.

Alisema wamefanya maombi hayo kwa lengo la kuwakabidhisha watoto hao mikononi mwa Mungu ili kuweza kufanya mitihani yao vizuri.

Alisema takribani wanafunzi 248 huku wasichana wakiwa 129 na Wavulana 119 ambao wanaotarajia kufanya mtihani wa darasa la saba katika Shule hiyo.

Kwa Upande wake Mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule hiyo,Leila Obunde alisema wamejiandaa vizuri na mtihani huo wa taifa na wanashukuru Shule hiyo kufanya maombi kwao.

“Maombi yaliyofanywa leo tunauhakika yatatufanya tufaulu vizuri kwa sababu wazazi watu wameshiriki maombi haya na kutuombea,” alisema

Aliongeza maandalizi ya darasani waliyoyafanya ni mazuri hivyo wanauhakika wa kufanya vizuri katika mitihani yao.