Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha akieleza jambo katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge kutoka Jimbo la Shanghai China.
………………
Na. Dianarose Shirima- Maelezo
Spika wa bunge la Shengai Yin Yicui,yuko nchini na wajumbe kumi na mbili wa bunge hilo ambapo jiji Dar es Salaam wamekutana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson Mwansasu kwa lengo la kubadilishana uzoefu mbalimbali kwa pande zote mbili. Spika Yin Yicui na wenzake wamefurahishwa na mapokezi na kusema kuwa baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Tanzania wakati alipotembelea Shengai, walifurahia kupata mwaliko huo na kuahidi kuja Tanzania.
Spika huyo aliongeza kuwa Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai limekuwa na uhusiano mzuri toka huko nyuma na kulenga kuendeleza maslahi mapana ya maendeleo ya Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai.
Katika mazungumzo yao wamejikita zaidi kuona jinsi wanavyoweza kushirikiana katika sekta ya elimu,mazingira na utunzaji wa maliasili na wanyamapori, ambapo watashirikiana katika hatua za utekelezaji.
Kwa upande wa mazingira, Bunge la Shengai linaangalia namna linavyoweza kusaidia uboreshaji wa mazingira, ambapowalipongeza serikali ya Tanzania kwa kupitisha sheria ya kupiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki na kuongeza kuwa, nchini kwao jimbo la Shengai wanajiandaa kupitisha sheria ambayo inahitaji utenganishi wa aina za takataka za majumbani. kwamba takataka za nyanya zisichanganywe na makopo. Dkt. Tulia aliongezea kuwa Tanzania inaangalia namna itakavyoitumia hiyo sheria ili kujifunza.
Naibu Spika aliwashukuru jinsi China wanavyoisaidia Tanzania kwa upande wa ufadhili wa masomo ya nje wanafunzi wanaotoka Tanzania, ambapo alisema ufadhili wao ni tofauti na ufadhili wa nchi nyingine, kwamba China huomba wanafunzi kwenda kusoma China wakati mataifa mengine wanafunzi huomba moja kwa moja katika nchi wanazopenda kusoma, pia katika vyuo vya VETA wataangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na Tanzania ikiwemo kusaidia vifaa vya kufundishia kama vile kompyuta
Mwisho walizungumzia namna ya Tanzania kutunza raslimali zilizopo nchini ambapo ni pamoja na wanyamapori na uoto wa asili, na kuahidi kuwa bega kwa bega na Tanzania ili kukuza na kuendeleza rasilimali za nchi.