Mwenyekiti wa jamii ya Kwanyama Mvumi Dodoma Mzee Yoram Mgua Mkuya
akimsimika uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) kuwa
Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu
mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika
kijiji cha Mvumi Dodoma.
Bibi Judith Javan Msonjela akimkabidhi vifaa vya uchifu Mzee Yoram Mgua
Mkuya akimsimika uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) baada ua kusimikwa kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.
Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Mzee John Samweli Malecela akitoa
baraka kwa Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) baada ua
kusimikwa kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi
iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika
Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.
Afisa Utamaduni Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Hadija
Kisubi akizungumza wakati wa hafla ya kusimikwa uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.
**********************
.
Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Jamii imeshauriwa kutunza na kulinda dhana za jadi zinazotambulisha utamaduni ili kuendelea kuenzi na kukuza mila na desturi ambazo ndio zinazotambulisha Taifa la Tanzania pamoja na kuweka kumbukumbu vizuri za jamii hizo.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Hadija Kisubi katika sherehe ya kusimikwa kwa Chifu wa Kabila la Wagogo Chifu Henry Mazengo iliyofanyika katika kijiji cha Mvumi Dodoma ambapo amesema kuwa jamii inapaswa kuhifadhi kumbukumbu zote za makabila yao kwakua ndio msingi wa utamaduni wa nchi.
“Taifa letu lina mila na desturi nzuri ambazo tunapaswa kuzilinda ,hivyo ni jukumu la kila jamii kuwa na makumbusho ambayo yatahifadhi mila na desturi lakini pia
itasaidia kukuza utalii wa kiutamaduni”alisema Bibi.Hadija.
Ameongeza kuwa Serkali inatambua mchango wa Machifu na viongozi wote wa kimila katika kuelimisha jamii tamaduni ambazo ndio kioo cha Taifa letu hivyo jamii
inapaswa kuzingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na Machifu hao.
Awali Mlezi wa Machifu Tanzania Mzee John Malecela amemshauri Chifu
aliyesimikwa Mzee Henry Mazengo kufuata taratibu za kabila hilo katika uongozi wake pamoja na kuendelea kuhimiza watu wa jamii yake kulinda amani ya nchi.
Naye Chifu Mazengo ameahidi kulinda mila na desturi za kabila la wagogo ambazo
zinaelekea kupotea kutokana na kabila hilo kuingiliana na makabila mengine lakini pia ameomba ushirikiano kwa ajimii yake ili kutimiza majukumu hayo vizuri.
Chifu Henry Mazengo amesimikwa kuwa Chifu wa pili Septemba 07,2019 kushika
nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 baada ya Chifu wa kwanza wa kabila hilo Chifu Chaula Mazengo kufariki dunia.