Wachezaji wa timu ya Sobibor wakisubiri mtanange kuanza kati ya timu hiyo dhidi ya Msewe baada ya kupokea muariko kushiriki Bonanza lililoandaliwa na Kikundi cha Born and Raised in Msewe kwaajili ya kuwakutanisha pamoja na kuunda ushirikiano.Bonanza hilo limefanyika leo mtaa wa Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam
Wachezaji wa timu ya Connection wakifuatilia mtanange kati ya Msewe dhidi ya Baruti katika Bonanza lililoandaliwa na Kikundi cha Born and Raised in Msewe katika Bonanza walioliandaa Kikundi hicho kwaajili ya kuwakutanisha pamoja na kuunda ushirikiano.Bonanza hilo limefanyika leo mtaa wa Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam
Wachezaji wa timu ya Baruti na Msewe wakichuana katika Bonanza lililoandaliwa na Kikundi cha Born and Raised in Msewe katika Bonanza walioliandaa Kikundi hicho kwaajili ya kuwakutanisha pamoja na kuunda ushirikiano.Bonanza hilo limefanyika leo mtaa wa Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam
Wakina mama wa Kikundi cha Born and Raised in Msewe wakicheza mchezo wa rede katika Bonanza walioliandaa Kikundi hicho kwaajili ya kuwakutanisha pamoja na kuunda ushirikiano.Bonanza hilo limefanyika leo mtaa wa Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam.
**************************
NA EMMANUEL MBATILO
Vijana wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kushirikiana kwenye masuala ya kijamii ili kuweza kuunda umoja ambao utakuwa na faida kwao na jamii hapo baadae.
Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Kikundi cha Born and Raised in Msewe (BRM) Bi.Regina katika Bonanza ambalo wameandaa kwaajili ya kuwakutanisha pamoja wanakikundi hicho.
Akizungumza na Fullshangwe blog katika Bonanza hilo Bi.Regina amesema kuwa Vijana wanatakiwa waunde umoja kwani kupitia mitandao ya kijamii imewafanya leo hii kuwa na ushirikiano wa kutosha na kusaidiana kwa mambo mbalimbali ya kijamii kwa kata ya msewe.
Aidha, Bi.Regina amewataka wakina wa mama wasiwe na tamaduni zilizopitwa na wakati kwa kuamini mazoezi ni kwa vijana wa kiume tu, hivyo amewataka wawaruhusu watoto wao wakike wajikite kwenye mazoezi kwani kuniweka kumsaidia kiafya.
“Nimependekeza bonanza hili kwa madhumuni ya kuwakutanishaaaa wanafamilia wa Born and raised in Msewe ili kutambuana pamoja na kushirikiana vizuri kwenye masuala ya kijamii kiujumla”. Amesema Bi.Regina.
Pamoja na hayo Bi.Regina ameongeza kuwa ameombwa kutengeneza kundi lingine kwaajili ya wanawake ili kuweza kushirikiana kwa pamoja na kutengeneza fursa ili kuweza kutatua Changamoto zao kama wanawake.
Kwa upande wake mmoja wa kiongozi wa Kundi hilo pia Bw.Fredrick Mayenja amesema kuwa uwepo wa Kikundi hicho wao wameweka utaratibu pindi mmoja wa familia ya Kikundi hicho anapopata matatizo hukutana kwa pamoja na kuona ni namna gani wanaweza kumsaidia.
“Tunawafundisha wado go zetu kuwa tu atakuwa kuwa wamoja kwani hata sisi baadae tunaweza kuwa wazee ndo maana wadogo zetu pamoja watoto wetu wamekuja kushuhudia Bonanza hili”.Amesema Bw.Mayenja.
Aidha amesema kuwa nje ya kusaidiana wao kama wao kwenye Kikundi, wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali kutatua Changamoto katika jamil kama barabara, uzoaji taka pamoja na shughuli nyingine.
Hata hivyo kwa upande wake Bw.Amosi Mkandawile amesema kuwa ushirikiano uliopo katika Kikundi hicho umekuwa na faida kubwa kwani kuna matatizo yamekuwa yakijitokeza kwa wanafamilia wa Kikundi hicho hivyo kwa pamoja ushirikiano kutatua tatizo.