Home Mchanganyiko RC MAKONDA ATOA KIBALI KWA WATUMISHI WA MUNGU KUTANGAZA INJILI SEHEMU ZA...

RC MAKONDA ATOA KIBALI KWA WATUMISHI WA MUNGU KUTANGAZA INJILI SEHEMU ZA CLUB NA DISKO.

0

**********************

Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 08 ametoa kibali kwa Watumishi wa Mungu wa Dini zote kuhubiri na kutangaza neno la Mungu kwenye Sehemu za Club, Disko na Kumbi za Starehe ili neno la Mungu lizidi kuenea na kuwafikia watu wote jambo litakalosaidia kujenga jamii inayomjua Mungu.

RC Makonda amesema Mtumishi wa Mungu atakapohitaji kuhubiri mziki utazimwa kwa muda wa Nusu saa na baada ya hapo watu wataendelea na starehe zao wakiwa tayari wamepokea Neno la Mungu na kuahidi kuwa Mmiliki wa Club atakaemkatalia Mtumishi Kuhubiri RC Makonda atamwombea Mtumishi huyo na ikibidi atamsindikiza.

Hatua hiyo ya RC Makonda imekuja baada ya kubaini uwepo wa Idadi kubwa ya watu kwenye sehemu za starehe na pindi watu hao wakienda Makanisani na Misikitini wanaishia kusinzia na wengine wanakuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kulisikiliza kwa ufasaha neno la Mungu.

Hayo yote yamejiri leo wakati alipokuwa akizungumza na Maelfu ya Wahumini wa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Mtumishi wa Mungu Apostle Boniface Mwamposa.