Home Michezo KASEJA AWA SHUJAA, TAIFA STARS IKIITUNGUA BURUNDI KWA MIKWAJU YA PENALTI

KASEJA AWA SHUJAA, TAIFA STARS IKIITUNGUA BURUNDI KWA MIKWAJU YA PENALTI

0

 

Shujaa wa timu ya Taifa ya Tanzania golikipa Juma Kaseja akibebwa juu juu na wachezaji wenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika ya timu ya Taifa ya Burundi na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kwenye uwanja wa Taifa ambapo Taifa Stars imepata ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Golikipa Juma Kaseja akionesha umwamba wake wa kupangua penati mbele ya mashabiki wa timu ya taifa huku akiwa amebebwa kwenye uwanja wa Taifa leo.

Kapteni wa timu ya taifa ya Tanzania na mchezaji wa timu ya Genk ya Ubelgiji akiongoza wachezaji wenzake kuingia uwanjani kabla ya kuchezo mchezo wao wa leo kufuzu fainali za kombe la Dunia 2022 nchini Qatar leo kwenye uwanja wa Taifa.

Mshabuliaji wa timu ya Taifa  na Kapteni wa timu hiyo Mbwana Samatta akiwachachafywa mabeki wa timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo.

Mshabuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na mchezaji wa timu ya El Jadid ya Morocco akiwania mpira na mabeki wa timu ya Burundi.

Mashabiki wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa ya Tanzania wakipasha.

Mwanamuziki Harmonize na Mkewe Sara walikuwa ni miongozi mwa mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars na timu ya Taifa ya Burundi leo kwenye uwanja wa Taifa.

*************************

Tanzania imefuzu hatua ya makundi leo kwa ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Baada ya dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 kisha zikaongezwa 30 nazo ngoma ikawa mbichi ya bila kufungana.

Timu zote zilianza kucheza kwa tahadhari na kushambuliana kwa zamu mpaka dakika 120 zinakamilika ngoma ilikuwa ni 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Tanzania ilikuwa ya kwanza kuandika bao lililofungwa na Mbwana Samatta dakika ya 29 na Burundi walisawazisha dakika ya 45 bao likiwekwa kambani na Mshambuliaji Abdul Fieston.

Kwa upande wa Tanzania wachezaji Erasto Nyoni, Himid Mao na Gadiel Mbaga waliweza kufunga huku Burundi wakikosa penalty zote.

Hii ilikuwa mechi ya marudiano baada ya kwanza kuchezwa nchini Burundi na timu zote mbili zikifungana 1_1.

Kwa Matokeo hayo Burundi wametolewa huku Tanzania ikiingia katika hatua ya Makundi ya timu nne zitakazowania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.