Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara
hiyo wakimsikiliza Mhandisi Issa Mohamed Issa wakati
akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya
Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima akisisitiza jambo wakati akipewa
taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara ya
Uhamiaji Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba 7,2019
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima (watatu kushoto) na baadhi ya
Wakurugenzi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza Mhandisi Issa
Mohamed Issa alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya
ujenzi wa jengo la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Mjini
Dodoma, Septemba 7,2019. (Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima (aliyekaa) akisisitiza jambo wakati
akipewa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Idara
ya Uhamiaji, Makao Makuu Mjini Dodoma, Septemba
7,2019 kutoka kwa Mhandisi Issa Mohamed Issa. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
***********************
Na Mwandishi Wetu-MOHA, Dodoma
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Ramadhani Kailima, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa
jengo la ghorofa 8 la Idara ya Uhamiaji Makao Makuu,
linalojengwa Mjini Dodoma.
Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 30 na unatarajiwa kukamilika
Novemba, 2020 ila unaweza kumalizika kabla ya muda huo
kama hakutatokea changamoto yoyote.
Kailima aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya kujionea
maendeleo ya ujenzi huo.
Jengo hilo linajengwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la
Kujenga Taifa (SUMA JKT).
Alisema ziara hiyo imelenga kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt.
John Magufuli juu ya kuhamia Dodoma.
Alifafanua kuwa, SUMA JKT ina Wakandarasi wazuri wenye
uzoefu mkubwa kwenye ujenzi wa majengo mbalimbali.
“SUMA JKT unapowapa mradi, ujenzi wake huwa unakamilika
kwa wakati ndio maana hupewa kazi nyingi za ujenzi wa
majengo ya Serikali,” alisema.
Kailima alisema hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye hatua ya
awali (chini), lengo la Serikali ni kuifanya Idara ya Uhamiaji
iondokane na uhaba wa majengo kwenye mikoa mbalimbali.
“Hivi sasa tunaendelea na ukarabati kwenye majengo ya
Uhamiaji Mtwara, Lindi, ukarabati mwingine utafanyika
Manyara,” alisisitiza Kailima.