Mkurugenzi wa Kampuni ya Kangaroo na Ndesoma akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kwenye kata ya Unga Ltd jijini Arusha picha na ahmed mahmoud arusha.
Magodown kwa ndani yanavyoonekana ambayo kampuni ya Kangaroo imekuwa ikiyataka ambayo yam ekaa bure bila kupangishwa kwa muda miezi mitatu sasa jambo ambalo limetokana na urasimu wa upangishaji kwa kudai bei kubwa huku bei elekezi ikiwapo picha zote na Ahmed mahmoud.
Sehemu ya nyaraka mbalimbali za mikataba ya pango la godown linalomilikiwa na kampuni ya Kangaroo ilayoilalamikia AICC kwa urasimu wa kuwaongezea Magodown mawili lakini kuna ukiritimba katika bei elekezi za manunuzi ya umma ambayo inajishughulisha na uzalishaji wa Raingi za viatu ambayo uwekezaji wake umegharimu kiasi cha milioni 500 picha na Ahmed mahmoud Arusha.
*******************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kituo cha kimataifa cha mikutano AICC kimetuhumiwa kwa kuendeleza kukwamisha juhudi za serikali za uwepo na uanzishaji wa viwanda nchini baada ya kuweka urasimu wa Kodi kubwa na mianya ya rushwa kwenye manunuzi ya umma kwa wapangaji wake kwenye Magodown yalipo eneo la Esso kata ya Unga Ltd jijini Arusha.
Akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho kinachotengeneze bidhaa mbali mbali ikwemo rangi za viatu aina ya Kangaroo Mkurugenzi wa kiwanda hicho Heladius Kanje alisema kuwa kutokana na ufinyu wa eneo aliomba kuongezewa eneo na ndipo alipoumba uongozi wa eneo hilo ambapo yeye pia ni mpangaji lakini bei aliyopewa haiendani na bei elekezi iliyopo.
Alisema kuwa magodown mawili yenye mita za mraba 384 anatakiwa kulipia kiasi cha tsh.590,000 pamoja na VAT kila moja kama bei elekezi lakini cha kushangaza nimetakiwa kulipia milioni moja laki tatu na elfu hamsini na tisa pamoja na VAT jambo ambalo nimekuwa nikizungushwa hadi sasa kupata eneo hilo.
Kwa mujibu wa Kanje alisema kuwa akiwa na Kampuni ya Kangaroo Nimeingia kupangisha nimekuwa nalipia kiasi cha milioni 1, na 057 lakini wenzangu walikuwa wakilipa kiasi cha 590,000 nilipoomba walikataa na kupandisha bei na magodwn mengine niliomba awali na kuwa milion 1,359,000 pamoja na VAT ambapo hadi sasa ni takribani miezi mitatu hayana wapangaji huu sio urasimu.
“Tokea niwe mkurugenzi hapa nimeanza na kampuni ya Ndesoma Indursty Ltd nimekuwa nalipia bei elekezi ya manunuzi ya umma kiasi cha 590,000 lakini cha kushangaza mara baada ya kuomba nalipia bei mpya kwa mwezi milion 1,359 Sisi tumewekeza karibu milion mia tano kwenye biashara huu ni urasimu mkubwa tunaomba serikali kuingalia hili kwetu sisi wajasiriamali tuliwekeza”alisema Kanje
Hata hivyo ameleeza kuwa aliomba kuongeza bei kutoka laki 5 hadi sita lakini amegundua sio fedha hizo wanaotaka bali kumekuwa na watu wenye urasimu wanaoishi kwa ten per senti jambo linalokwamisha kufikia malengo yetu na serikali kwenye uchumi wa kati wa viwanda.
Akamuomba waziri wa viwanda na biashara kufika kwa haraka kujakuona jinsi wadau wa serikali katika kufikia Tanzania ya viwanda wanavyokwamishwa kuwekeza na viongozi waliopewa dhamana ndani ya serikali wakati mh.Rais anapiga kelele hapendi kutawala watanzania wanaolia kila uchwao.
Waandishi wa habari walishudia eneo hilo la uwekezaji ambalo mwekezaji mzawa anataka kuwekeza lipo kwenye hali mbaya ya uchakavu na kuvuja jambo ambalo halipo kwenye taswira ya uwekezaji inayotakiwa na inahitajika kulifanyia ukarabati.