Baadhi ya wafanyabiashara wakifurahia jambo wakati wa kongamano la wanachama wa klabu ya wafanyabiashara mkoa wa Tabora uliolenga kuwapa mafunzo na nidhamu ya biashara. Kongamano hilo liliandaliwa na Benki ya NMB kuwapa elimu na fursa zakukuza biashara zao kupitia benki hio.
……………………
Na: Mwandishi wetu,Tabora
Wafanyabiashara katika Mkoa wa Tabora,wengi hawajilipi mishahara kutokana na kazi zao wanazofanya na hivyo kukosa fursa ya kufahamu namna biashara zao zinavyokua au zinavyodorora.
Haya yamebainishwa na Meneja wa NMB kanda ya Magharibi, Sospeter Magese,wakati akizungumza na wafanyabiahara wa Mkoa wa Tabora, alisema wengi huwa hawajilipi mishahara na kufanya mahesabu yao kutokuwa vizuri.
“Inashangaza mfanyabiashara anawalipa wafanyakazi wake mshahara lakini yeye akiwa mkurugenzi hajilipi mshahara na pia huchanganya matumizi binafsi na ya biashara jambo amvalo huyumbisha mitaji yao.
Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya wafanyabiashara juu ya huduma inayotolewa na NMB, Magese aliwaeleza kuwa kupitia mishahara yao ndio matumizi ya binafsi yanaweza kutoka huko na sio katika biashara.
Aliwaeleza kuwa benki ya NMB ni benki yao na waitume kwani imejipanga kushirikiana nao katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wenye akaunti benki ya NMB,Ahadi Mviombo,aliwahimiza wafanyabiashara kutenga sehemu ya mauzo yao kwa ajili ya kulipa madeni wanayokopa.
“Kama ukiweza kutenga angalau shilingi elfu tano kila siku kwa ajili ya marejesho mtihani utakuwa umeshinda”Alisema
Mfanyabiashara Mwalimu Mambo,aliipongeza NMB kwa utaratibu wake wa kuwafundisha wafanyabiashara namna ya kuweka mahesabu sawana kutafuta faida.
“Tunashukuru kwa elimu tunayopewa na benki hii ambayo kwa kweli inatusaidia sana katika biashara zetu”Alisema
Kikao hicho chenye lengo la kupokea maoni kutoka kwa wafanyabiashara ziadi ya 300 wenye akaunti NMB pia kilihudhuriwa na wafanyakazi wa benki hiyo ambao walitoa elimu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.