Wachezaji wa Uholanzi wakipongezan baada ya ushindi mzuri wa ugenini wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Ujerumani usiku wa jana Uwanja wa Volkspark mjini Hamburg katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro ya mwakani. Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Frenkie de Jong dakika ya 59, Jonathan Tah aliyejifunga dakika ya 66, Donyell Malen dakika ya 79 na Georginio Wijnaldum dakika ya 90 na ushei, wakati ya Ujerumani yalifungwa na Serge Gnabry dakika ya tisa na Toni Kroos kwa penalti dakika ya 73 PICHA ZAIDI SOMA HAPA