Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe (95) amefariki dunia katika hospitali ya nchini Singapore akipambania afya yake.
Mugabe atakumbukwa kwa mazuri aliyoyafanya kwenye nchi yake hasa katika kupigania uhuru dhidi ya Wakoloni mpaka pale alipachaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo mwaka 1980 na baadae mwaka 1987 kuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo ya Zimbabwe.
Mugabe aliondolewa madarakani kwa ngumu za kijeshi Novemba 2017 baada ya kukaa madarakani takribani miaka 37.
Mhasibu wa nchi ya Zimbabwe Fadzayi Mahere ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter “Rest in Peace, Robert Mugabe”.