Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Zainabu Matitu Vullu akizungumza na wakazi wa Dimani kabla ya kukabidhi Vifaa kwa ajili ya kambi za wanafunzi wa shule ya msingi.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Zainabu Matitu Vullu akikabidhi Taulo kwa ajili ya watoto wa kike wanaojiandaa na Mtihani wa Darasa la Saba.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Zainabu Matitu Vullu akikabidhi penceli na vifutio kwa wanafunzi wanaotaraji kufanya Mtihani wa Darasa la Saba kata ya Dimani Wilayani Kibiti.
…………………
Na Mwandishiwetu
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT), Zainabu Matitu Vullu ametoa Vifaa na vyakula vyenye thamani Milioni mbili laki nane kwa wanafunzi wa Darasa la Saba waliopo kambini katika shule za Kata za Dimani,Kibiti na mwambao wilayani Kibiti.
Akizungumza na wananchi waliokusanyika katika kata ya Dimani alisema shule zote hizo Zina wanafunzi 838 ambao wapo kambini kwa ajili ya Mtihani wa Darasa la Saba utakaofanyika Septemba 12 ,2019.
“Kwa upande wangu nimeona nitoe Vifaa hivi penceli vifutio, Taulo za kike pamoja na vyakula ambavyo ni sembe, Mchele, dagaa na Maharage hili viweze kuwasaidia Vijana Hawa katika maandalizi bila ya kuwapa presha wazazi ” Amesema Vullu
Amesema kuwa msaada huo ambao umewalenga watoto wote hao ni vyema wakaanza kupatiwa wanafunzi wale ambao wapo katika mazingira hatarishi na wamekuwa awana uhakika wa kupata chakula na Vifaa vya kufanyia Mtihani.
Mbali ya Vifaa hivyo Mh Zainabu Matitu Vullu ametoa msaada wa mashuka kumi kwa ajili ya Zahanati ya kata ya Dimani pamoja na jola moja kwa ajili ya mapanzia ya Zahanati hiyo.
Amesema kuwa amepita katika Zahanati hiyo na kujionea hali halisi hivyo kwa kuanzia ametoa Vifaa hivyo hili kufanya mazingira yapo kuwa ya kuvutia.
Mh Vullu amewataka wazazi wa wanafunzi hao kuandaa mazingira Bora ya Vijana wao kuendelea na shule na kuacha kuwanunulia vijana bodaboda na kuozesha watoto wa kike mapema .
Alimaliza kwa kuwashukuru walimu wanaowafundisha Vijana hao na kuwataka wasikate tamaa kwani ufaulu wa watoto hao upo mikononi mwao hivyo wao kama Viongozi ni kuweka mazingira wezeshi.