*******************
Na Mwandishi Wetu
Wimbo mpya wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msanii Peter Msechu, umeteuliwa
kuwa wimbo maalum katika Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki
linalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Septemba 21-28 mwaka huu katika Uwanja
wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za wimbo wa JAMAFEST2019 kuteuliwa kuwa wimbo rasmi wa Tamasha hilo
maarufu Afrika Mashariki zilifahamika baada ya Msechu kuandika katika ukurasa
wake wa Instagram akimshukuru Mungu kwa wimbo wake huo kupitishwa.
Akiongea baada ya kupigiwa simu kutoa ufafanuzi juu ya kuchaguliwa kwa wake
kuwa kuwa maalum katika tamasha la JAMAFEST, Msechu alisema kuwa alitunga
wimbo huo baada ya uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kuwaomba wasanii mbalimbali kutunga wimbo ambao ungetumika kama wimbo
maalum wa Tamasha.
“Wasanii tupo wengi sana kwa mimi kupata fursa hii ya kuimba katika ufunguzi
tamasha hili kubwa la JAMAFEST kwangu ni heshima kubwa sana. Tulikuwa wasanii
wengi tuliotunga nyimbo kwa ajili ya Tamasha lakini wimbo wangu umechaguliwa
ni furaha kubwa”, alieleza Msechiu.
Amesema kwa sasa anaandaa video ya wimbo huo ili uweze kutumika kuhamasisha
watanzania na watu wa Afrika Mashariki kushiriki katika Tamasha ambalo lengo la
kudumisha uridhi wa utamaduni, Sanaa za mikono na ubunifu, biashara na kukuza
Akiongea kuhusiana na Wimbo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST, Bi. Joyce Fissoo alisema kuwa mchakato wa uteuzi wa wimbo rasmi kwa ajili ya Tamasha la JAMAFEST haukuwa rahisi kwani kulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na wasanii wengi wakujitokeza na kufanya utunzi wawimbo kwa ajili ya tamasha .
“Mchakato wa kupata wimbo wa Tamasha ulikua mgumu kutokana na wasanii
kujitokeza na baada ya kusikiliza nyimbo zote ndipo Sekretarieti ya Maandalizi ya
Tamasha inayoundwa na Wajumbe kutoka nchi sita wanachachma wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki ikauchagua wimbo wa JAMAFEST2019 ulioimbwa na Msechu kuwa
ndio wimbo wa tamasha”, alieleza Bi. Fissoo.
Tamasha la JAMAFEST ni tamasha lililopitishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya
Afrika Mashariki ili kuenzi na kulinda utamaduni wa makabila ya Afrika Mashariki.
Tamasha hili hufanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi wanachama ambapo
mwaka huu tamasha hilo litafanyika nchini Septemba 21-28 katika Uwanja wa
Taifa.