Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,Dk.Juma Abdallah Saadala “Mabodi”, (Katikati) Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,Jana, Muda Mchache Kabla ya Viongozi wa Chama Hicho Kuanza Safari Kutoka Nchini Kuelekea Nchini China kwa Ziara ya Siku 10 Huku Msafara Huo Ukiwa na Ujumbe wa Viongozi 20 wa Chama Hicho Kutokea Tanzania Bara na Visiwani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Erasto Sima na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Jumuiya ya Chama Hicho Taifa,Mwalimu Queen Mlozi. Picha na Elisa Shunda
……………….
NA:ELISA SHUNDA,DAR
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kuendelea Kujenga Mahusiano Mazuri na Nchi Mbalimbali Kupitia Vyama Rafiki za Nchi Hizo Zenye Mlengo Sawa wa Kisiasa wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea Duniani.
Hayo Yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,Dk.Juma Abdallah Saadala “Mabodi”, Wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam,Jana, Muda Mchache Kabla ya Viongozi wa Chama Hicho Kuanza Safari Kutoka Nchini Kuelekea Nchini China Ambapo Msafara Huo Unaongozwa na Kiongozi Huyo Umeondoka na Wajumbe Takribani 20 Kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha Dk.Mabodi Aliiongeza kwa Kusema Ziara Hiyo ya Siku Kumi ni Moja Kati ya Ziara Ambazo Huwa Zinafanywa Baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama Rafiki cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa Ajili Kudumisha Urafiki Ulioasisiwa na Viongozi Wawili wa Mataifa Hayo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Zedong Ambao Walikuwa na Imani Moja katika Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Aliongeza kwa Kusema Ziara Hiyo Italeta Manufaa kwa Chama na Taifa kwa Ujumla Kutokana na Kauli Mbiu ya Hapa Kazi Tu Inayohamasisha Utendaji Kazi Wenye Tija kwa Maendeleo ya Nchi Yetu Inayotekelezwa Ilani ya CCM na Serikali ya Awamu ya Tano Inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli Kutokana na Uwajibikaji Mzuri wa Rafiki Zetu Wachina Viongozi Hao Watajifunza na Kujionea Maendeleo Mbalimbali Ambayo Watawasilisha Mawazo Yao Nchini Nini Kifanyike.
“Kwa Sasa Nchi Yetu Kupitia Mwenyekiti wa CCM Taifa,Jemedari Wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Magufuli katika Kauli Mbiu Yake ya Hapa Kazi Tu, Ni Imani Yangu Mimi na Wenzangu Tutajifunza Vitu Vingi Ambavyo Vitakuwa na Tija kwa Taifa Letu Lakini Pia Ukiachia Urafiki Baina ya Chama cha CCM na CPC ya China Pia kwa Sasa Tupo katika Mchakato wa Ujenzi wa Viwanda Vikubwa na Vidogo, Wote Tunafahamu Wenzetu China kwa Sasa Wako Juu katika Utengenezaji wa Bidhaa Mbalimbali Duniani;
“Hivyo Kwetu Kama Viongozi ni Fursa Nzuri Ambayo Itatufanya Tujifunze Juu ya Uendeshaji wa Viwanda na Ubunifu katika Uzalishaji katika Viwanda Vidogo na Utendaji Kazi Wake, Lakini Pia Tupo katika Mchakato wa Ujenzi wa Reli ya Mwendo Kasi Kutoka Dar Hadi Dodoma kwa Awamu ya Kwanza Kuna Uwezekano Awamu ya Pili Serikali Ikawapatia Ndugu Zetu Wachina Waendelee na Ujenzi Huo kwa Awamu ya Pili Tunatambua Mchango Wao katika Ujenzi wa Reli ya Tazara, Hivyo Ziara Yetu kwa Viongozi Sisi 20 Italeta Manufaa kwa Chama Chetu na Serikali kwa Ujumla Wake” Alisema Dk.Mabodi.
Aidha Katika Msafara Huo wa Viongzo 20 Wanaongozwa na Naibu Katibu CCM Zanzibar,Dk.Mabodi, Pia Wameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Erasto Sima,Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Jumuiya ya Chama Hicho Taifa,Mwalimu Queen Mlozi,Wenyeviti wa CCM Mikoa Akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu na Wajumbe Wengine Jumla Kuu Yao Ishirini.