Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Ndumbaro akiwa kwenye ndege ya Air Tanzabia na wanasheria walipambana kisheria katika Mahakama ya Gauteng nchini Afrika Kusini na kufanikisha ndege hiyo iliyokiwa inazuiliwa nchini humo kuachiwa.
****************
NA EMMANUEL MBATILO
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Damas Ndumbaro ameongoza safari ya kurudi nchini Tanzania baada ya kuachiwa kwa Ndege ya Air Tanzania ilipokuwa imeshikiliwa nchini Afrika Kusini.
Akizungumza baada ya kuachiwa kwa ndege hiyo Dkt.Ndumbaro amesema kuwa Tanzania tayari imelipa zaidi ya dollar millioni 20 kwa ushahidi wa kutosha kwa mlalamikaji aliyezuia ndege ya Tanzania nchini Afrika kusini katika deni ambalo lilikua ni jumla ya millioni 30.
“Bw.Steyn alikuwa ameshalipwa dola milioni 20 za kimarekani kwa hukumu ile ile kwa hiyo sio kwamba serikali ya Tanzania haikulipa, ila sasa alichokifanya ni badala ya kufuata hukumu ya mahakama kuu nchini Tanzania,aling’ang’ania maoni kati ya mwanasheria mmoja kwamba hukumu moja haiwezi kumfunga”. Amesema Dkt.Ndumbaro.
Aidha Dkt.Ndumbaro amesema kuwa mlalamikaji ameshauriwa kuwa arudi nchini Tanzania ili aweze kuruhusu au kuwezesha akiba yake ambayo bado hajalipwa badala yakuendelea kukaa na kuzunguka kwenye mahakama tofauti tofauti.
Kufuatia maamuzi ya mahakama nchini Africa kusini ya kuachiwa kwa ndege ya Tanzania, wanasheria wamedai kuwa wamecheleweshwa vyakutosha japokuwa tayari mlalamikaji amelipwa zaidi ya milioni 20 dola za kimarekani kati ya milioni 30.