Home Mchanganyiko Benki ya BancABC Yatoa Msaada wa Mazishi wa Mteja Wake wa Mkopo...

Benki ya BancABC Yatoa Msaada wa Mazishi wa Mteja Wake wa Mkopo Rahisi Dar es Salaam

0

Meneja wa benki BancABC Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni (aliyesimama) akiongea wakati wa kukabidhi rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa mke wa mmoja ya mteja wa Mkopo Rahisi ambaye alifariki kwenye tukio lilofanyika jana (leo) jijini Dar es Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu.

Meneja wa benki ya BancABC Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni akikabidhi hundi ya Tzs500,000/- kwa Maria Privatus ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam baada ya kufiwa na mume wake. BancABC Tanzania kupitia Mkopo Rahisi ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa pole kwa familia ya mteja wake pale anapofariki akiwa na na Mkopo Rahisi kutoka benki hiyo. Anayeangalia ni Ofisa Mikopo wa benki hiyo Ally Bendera.

Mnufaika wa Mkopo Rahisi Maria Privatus akionyesha hundi baada kukabidhiwa na BancABC leo jijini Dar es Salaam. Mkopo Rahisi ni mkopo ambao utolewa na BancABC ambapo mteja anapofariki benki hiyo ufuta deni la mkopo pamoja na kutoa rambi rambi ya Tzs500,000/- kwa familia ya marehemu

…………………….

Benki ya BancABC ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania imetoa msaada wa mazishi kwa Mke wa mmoja wa wateja wake wa Mkopo Rahisi wa jijini Dar es Salaam ambaye hivi karibuni alifiwa na mume wake. Mkopo Rahisi ni moja ya huduma ambayo hutolewa na BancABC kwa ajili ya kufariji familia ya mteja wake inapotokea kifo kwa kufuta mkopo uliokuwa umebaki pamoja na kutoa msaada wa Tzs500,000/- kwa familia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa Maria Privatus ambaye mume wake alikuwa ni mteja wa BancABC Mkopo Rahisi kabla ya kufariki, Meneja wa BancABC Kanda ya Dar es Salaam Ferdinand Mgeni alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa msaada kwa familia ambayo mteja alikuwa na Mkopo Rahisi kutoka BancABC. ‘Kile ambacho mnaona tukifanya hapa leo ni jambo ambalo tulikuwa tukifanya siku zote. Sisi BancABC ambao ni kampuni tanzu ya Atlas Mara Tanzania tuliamua kuwa na kipengele cha aina hii kwenye mikopo yetu ya Mkopo Rahisi ili tuwe tofauti na wengine kwenye soko. Lakini zaidi ni kufanya familia ya wafiwa kuwa na amani kwani mbali na kutoa rambi rambi ra Tzs500,000/- lakini pia tunafuta deni la mkopo ambao marehemu alikuwa anadaiwa, Mgeni aliongeza.

Mgeni aliongeza kuwa mkopo wa Mkopo Rahisi unao faida nyingi kwa mteja kwani una riba ya chini kwa mwezi. Nia yetu ni kupunguza mzigo kwa wateja wakati wa kulipa mikopo yao. Vile vile Mkopo Rahisi unatoa muda mrefu wa kulipa kwani muda wake ni miezi 72 (miaka 6) na wateja anaweza kupata mkopo hadi TZS40 milioni.

Naomba nichukue fursa hii kuwaomba Watanzania kutembelea tawi lolote la BancABC na kupata mkopo wa Mkopo Rahisi ambao ni rahisi na haraka kupata. Wateja wetu wanao uhuru wa kutumia mkopo kwa uhuru wao iwe ni kulipa ada ya shule, kodi ya nyumba na mengineo lakini pia muda wowote mteja anaweza akiongezea kuchukua mkopo wake.

Akizungumza baada ya kupokea rambi rambi hiyo ya Tzs500,000/-, Maria Privatus ambaye mume alifariki akiwa ni mwalimu wa shule ya wasichana ya Zanaki ya jijini Dar es Salaam alisema, ‘Nawashukuru sana BancaABC kwa kutoa muda wenu na kuja kunitembelea pamoja na kunipa rambi rambi hii. Nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza chakula hapa shuleni ambapo mume wangu alikuwa ni mwalimu. Nitatumia pesa hii kwa ajili ya kukuza biashara yangu na hatimaye niweze kuendesha familia kwani kwa sasa nimebaki bila ya kuwa na mtu wa kunisaidia.

Maria aliongeza, kwa sasa mimi nishahidi mzuri wa BancABC. Wakati kutangaza kwamba mteja wenu wa Mkopo Rahisi anapofariki, benki mara moja ufuta deni la mkopo wake pamoja na kusaidia familia ya marehemu kwa kiasi cha Tzs500,000/- sikuamini mpaka haya ya kwangu yalipotokea. Nitaendelea kuwa mteja wenu na nawaomba Watanzania wajiunge na BancABC kwani ni benki yenye bidhaa na huduma za uhakika kwa hapa nchini.