Na.Alex Sonna,Dodoma
BUNGE limeelezwa kuwa afya za wanawake wengine Vijijini zinaathiriwa na moshi wa kuni wanapopika kwenye majiko ya mafiga matatu ambayo yanatumia kuni nyingi na hivyo kuchochea kasi ya ukataji miti.
Hayo leo bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Shally Raymond wakati alipokuwa akiuliza swali kuhusu mpango wa kuondoa majiko ya mafiga matatu.
Katika swali lake la kwanza alihoji Je,Serikali ina mpango gani wa kuondoa matumizi ya majiko ya mafiga matatu kote nchini na Swali lake la pili a Je,serikali ina mkakati gani wa haraka wa kuondoa majiko hayo kwenye shule zote za msingi na sekondari.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amesema kuwa matumizi ya tungamotaka hususan kuni na mkaa kama chanzo cha nishati ya kupikia nchini yanakadiliwa kufikia asilimia 85.
“Matumizi ya tungamotaka ikiwemo mafiga matatu husababisha madhara ya kiafya kutokana na kuvuta hewa chafu inayotokana na kuni na mkaa kwa watumiaji pamoja na uharibifu wa mazingoira kutokana na ukataji wa miti”amesisittiza.
Aidha Mhe.Mgalu amesema kuwa kupitia sera ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015,serikali imekuwa ikihamasisha matumizi bora ya Nishati ikiwemo teknolojia zinazopunghuza gesi ya ukaa na matumizi makubwa ya kuni na mkaa kwa kutumia majiko banifu.
Amesema kuwa Serikali imekuwa ikihamasisha kuacha matumiz ya nishati mbadala wa kuni na mkaa katika kupikia na gesi za mitungi,bayogesi,vitofali vya mabaki ya tungamotaka na majiko ya nishati ya jua.
“Wakal wa Nishati Vijijini (REA) kupitia mfuko wa nishati vijijini pamoja na jukumu la usambazaji wa teknolojia bora za kupikia hususani katika taasisi za umma nchi nzima zikiwemo shule,Magereza,kambi za wakimbizi na zahanati.”amefafanua