Home Biashara VIJANA 500 BAGAMOYO KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

VIJANA 500 BAGAMOYO KUPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI

0

Vijana zaidi ya 500 wilayani Bagamoyo wanatarajiwa Kunufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Kambi maalum itakayofanyika mwezi Septemba Katika Kijiji cha mandera Wilayani Bagamoyo.

Kambi hiyo iliyopewa jina la “Kambi Moto” inatarajiwa kufanyika kwa siku 10 na itaanza rasmi Septemba 3, mwaka huu na kufunguliwa na Katibu wa UVCCM Taifa, Mwl Raymond Mwangala ambapo pamoja na Mafunzo ya ujasiriamali, vijana hao watashiriki Shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi wa Darasa pamoja na Kuanza Ujenzi wa ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi wilayani humo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi Uvccm, Mkwayu Makota, amewataka Vijana kuchangamkia Fursa hiyo kwakua mafunzo hayo yatawaongezea maarifa mengi yatakayowasadia Kujiajiri.

“Tunawashukuru sana Viongozi wetu wa ngazi zote Za Vijiji,Madiwani ,Wabunge na Wakurugenzi pamoja na mkuu a Wilaya kwa namba wanavyotupa Kipaumbele Vijana hasa kwenye Kupigania Mikopo ya Vijana nasi kama Umoja wa Vijana tumeona ni vyema Tuanzishe Kambi hii ili kuzidi kuongezeana maarifa ” alisema Mkwayu Makota