Home Mchanganyiko TBL Mbeya yatoa msaada wa vitendea kazi mashuleni

TBL Mbeya yatoa msaada wa vitendea kazi mashuleni

0

Walimu kutoka shule mbalimbali wakiangalia Printer zilizotolewa na TBL

Meneja wa kiwanda cha TBL cha Mbeya, Godwin Fabian, akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Printer mashuleni mkoani Mbeya

Mmoja wa walimu akipokea msaada wa Printer.

…………………………………………………….

Katika mwendelezo wa kutekeleza sera yake ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kijamii katika sekta mbalimbali, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya kampuni mama ya Kimataifa ya AB InBev, imetoa msaada wa Printer 12 zenye thamani ya zaidi ya milioni 50 kwa shule za msingi na sekondari mkoani Mbeya.

Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika mkoani Mbeya na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa TBL na watendaji mbalimbali kutoka sekta ya elimu.

Meneja wa kiwanda cha TBL cha Mbeya, Godwin Fabian, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za  kupambana na changamoto mbalimbali kwenye jamii hususani katika sekta ya elimu kama ambavyo imetoa msaada huo wa Printer kwa ajili ya kurahisisha kazi mashuleni