Katibu wa UVCCM mkoa wa Katavi Theonas Kinyonto akizungumza na waandishi wa habari
………………….
Na Mwandishi wetu, Katavi
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Katavi umempongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mikubwa mkoani Katavi
Akitoa pongezi hizo Katibu wa UVCCM mkoa bwana Theonas Kinyonto amesema ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mpanda hadi Tabora unaashiria utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/20
Aidha kupitia mradi wa uboreshaji miji utekelezaji wa mradi wa barabara ya lami ya kilometa 7.7 katika manispaa ya Mpanda uliogharimu shilingi bilioni 8 ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimi 97
Pia wamemsukuru Rais kwa kutoa fedha za kujenga kituo kikubwa cha mabasi halikadhalika kuboresha miundombinu ya afya katika mkoa wa Katavi sanjari na ujenzi wa Hospitali za Wilaya tatu katika mkoa wa Katavi
Katika hatua nyingine bwana Kinyonto ametoa wito kwa Vijana kujiunga katika makundi ili kupata mikopo ya Halamshauri ambapo jumla ya shilingi milioni 700 zimetengwa kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kuwezesha makundi mbalimbali
Pia amepongeza suala la kutolewa kwa elimu bure jambo ambalo limeongeza uandikishaji wa wanafunzi mashuleni ambapo pia amewashukuru wazazi kwa kujitolea nguvu zao katika kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa
Aidha amewakumbusha vijana kuwa kupitia miradi yote inayotekelezwa na serikali ni fursa za ajira kwa vijana hivyo hawana budi kuzitumia fursa hizo vizuri