************
Na Judith Mhina – Maelezo
Kitendawili cha miongo kadhaa iliypita ambacho Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaambia Watanzania “Fedha sio Msingi wa Maendeleo,” mara baada ya Uhuru, huenda halikueleweka vema kwa wakati huo, kutokana na idadi ya wasomi kuwa wachache.
Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji vitu vinne yaani Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora na kupinga dhana ya wengi wakati huo na mpaka sasa kuwa. “Fedha ndio Msingi wa Maendeleo”. Bali fedha ni matokeo ya Juhudi, ubunifu na maarifa unayoyatumia katika kutumia rasilimali uliyonayo kufanikisha kilichokusudiwa na mtu, familia moja moja na Taifa kwa ujumla ndipo upate fedha.
Maneno hayo yamewekwa bayana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Sita la Uongozi Afrika kwa Marais Waastaafu lililofanyika Ikulu – Jijini Dar-es- salaam kwa muda wa siku mbili hivi karibuni.
Akifungua Mkutano huo, Rais Magufuli amesema “Kushindwa kusimamia maliasili zetu na kuleta maendeleo kwa watu, tumedanganywa tukidhani “Fedha ndio msingi wa maendeleo, bali fedha ni matokeo ya mikataba na makubaliano tuliyoingia na wawekezaji katika kutumia rasilimali zetu”.
Mara nyingi mikataba hii hunufaisha upande mmoja, the agreement are not found in the win win principle, tatizo hili limesababisha matumizi mabovu ya maliasili za Afrika bila kuleta matokeo chanya kwa wakazi wa bara hili.
Amesema Rais Magufuli Chanzo kikubwa cha mikataba mibovu Rais Magufuli amesema kuwa ni ukosefu wa uzalendo miongoni mwa watendaji wa serikali zetu na hujuma zinazofanywa na mabeberu pamoja na vibaraka wao wa ndani ya nchi
husika.
Endepo watendaji wetu wangekuwa na uzalendo na sisi wanasiasa pia wasingekubali kuingia mikataba isiyo na manufaa kwa mataifa yao.
Akisisitiza kuwa fedha ni matokeo ameongeza kwa kusema “As Africans we must focus on what is available in our local and immediate context and transform it into money. Fedha ni matokeo ya mwisho kabisa ya matumizi ya maliasili zetu na sio msingi wa Maendeleo”.
Akitaja baadhi ya rasilimali hizo zinazozaa fedha Rais Magufuli amesema kuwa ni kama vile, ardhi, madini mafuta, gesi, hifadhi, maeneo ya misitu na maeneo yanayofaa kwa kilimo duniani ambapo takribani asilimia 30 ya ardhi yenye rutuba duniani inapatikana Barani Afrika.
Hata hivyo rasilimali hizo hazijasimamiwa kikamilifu ili ziliete manufaa ya kiuchumi ambapo, msingi mkubwa wa maendeleo ni rasilimali hizo ikiwani pamoja na watu ambao tunao. Lakini uwepo wa rasilimali na watu wake havitoshi iwapo hakuna mifumo bora ya kusimamia rasilimali na kuwaendeleza watu ili waweze
kusimamia hizo rasilimali.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alilitambua hilo ndio maana alitamka ili tuendelee tunahitaji mambo manne ikiwemo “Uongozi Bora” ambao utaweka mifumo bora na thabiti, ambayo itahakikisha njia zote kuu za uchumi zinakuwa mikononi mwa wananchi wa Tanzania ahadi ya chama tawala wakati huo Tanganyika African
National Union-TANU.
Kazi kubwa ya kuwaendeleza watu ili kusimamia rasilimali ilianzishwa na Awamu ya Kwanza ya uongozi chini ya Mwalimu Nyerere kwa kuzingatia elimu ya kujitegemea ili kuwa na Uhuru wa kweli. Elimu ambayo kila mtanzania aliyeipata atakuwa tayari kuitumia kwa manufaa ya watanzania wote kwa kuwa na mifumo sahihi
ya kusimamia rasilimali zilizopo kwa manufaa ya nchi, sio Uhuru wa kudhani waliotutawala (wakoloni) watatusaidia.
Rais Magufuli amekuwa Mwalimu mkweli na muwazi kwa kuwakumbusha Watanzania kuwa alichosema Mwalimu Nyerere tuwaache Watanzania wakijitambua na kupata maarifa watatumia rasimali zao kwa faida yao hapo baadaye. Kinyume chake kutokana na mifumo isiyo mizuri rasilimali hizo zimekuwa zikiwanufaisha wengine badala ya wahusika.
Akionyesha madhara yatokanayo na fikira hizo za wakoloni Rais Magufuli amesema “Masalia ya fikira za kikoloni hatukutafsiri vizuri dhana ya uhuru hii ina maana uhuru na kujitegemea kama hujitegemei huwezi kuwa huru. Nadhani watawala wetu waliotutawala ndio mwanzo wa ugonjwa wa kuwa tegemezi dependency syndrome unaolitesa Bara la Africa Utegemezi huu ndio umeimarisha misingi ya ukoloni mamboleo”.
Wapo wengi ambao hawakumuelewa Mwalimu Nyerere wakati ule, ambapo limerejelewa na kutolewa mifano kadhaa ambapo, nina hakika somo limeeleweka kuwa fedha sio Msingi wa Maendeleo bali ni matokeo ya mwisho kabisa ya matumizi ya rasilimali ikiwemo maliasili zetu. Amesema Rais Magufuli.
Akielezea mifumo inayotumiwa na rasilimali watu Barani Afrika inayodidimiza uchumi wa Afrika Rais Magufuli amesema kuwa mikataba na makubaliano yanayongia na wawekezaji katika kutumia rasilimali zetu mara nyingi mikataba hii hunufaisha upande mmoja. The agreement are not found in the win win principle tatizo hili limesababisha matumizi mabovu ya maliasili za Afrika bila kuleta matokeo chanya kwa wakazi wa bara hili.
“Chanzo kikubwa cha mikataba mibovu ni ukosefu wa uzalendo miongoni mwa watendaji wa serikali zetu na hujuma zinazofanywa na mabeberu pamoja na vibaraka wao wa ndani ya nchi hisika. Endepo watendaji wetu wangekuwa na uzalendo na sisi wanasiasa pia wasingekubali kuingia mikataba isiyo na manufaa kwa mataifa yao”.
Akionyesha madhara yatokanayo na fikira hizo za wakoloni Rais Magufuli amesema kuwa masalia ya fikira za kikoloni hatukutafsiri vizuri dhana ya uhuru hii ina maana uhuru na kujitegemea kama hujitegemei huwezi kuwa huru. Nadhani watawala wetu waliotutawala ndio mwanzo wa ugonjwa wa kuwa tegemezi dependency syndrome unaolitesa Bara la Africa Utegemezi huu wa kuomba misaada ya fedha kila uchweo ndio umeimarisha misingi ya ukoloni mamboleo.
Akihitimisha hotuba yake katika suala zima la Akitambua Ukosefu wa ubunifu na tekinolojia ya viwanda lack of innovation and Industrial back awareness haitaweza kusimamia na kutumia rasilimali zake kiendelevu bila kuwa na viwanda lazima tukuze ubunifu kwa vijana wetu.
kuwa vijana ni nguvu kazi inayotegemewa na Taifa amesema kuwa lazima vijana wajikite katika tekinolojia rahisi na kufanya uhaulishaji wa tekinolojia ya viwanda ndani ya bara letu. Ili tuweze kusindika asilimia kubwa ya mazao yanayotokana na maliasili zetu, tusiendelee kuuza malighafi za kilimo, misitu, madini, mifugo na
uvuvi bila kuongeza dhamani.
Pia, ameangalia migogoro na hali tete ya kisiasa Barani Afrika, ambapo maeneo mengi katika bara letu hususani yenye maliasili nyingi yanakumbwa kwa sehemu kubwa migogoro hii inatokana na mabeberu wanaotaka kuendelea kutumia maliasili hizi kwa manufaa yao. Wakati sisi tunapigana wao wanakula na
kamwe hawatapenda mataifa yetu yawe na amani kwani migogoro ndio mtaji wao. Ametaarifu Washiriki na Umma Rais Magufuli.
Akihitimisha Mkutano huo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa amesema “Hasira ya kutumia rasilimali kwa maendeleo ya Afrika lazima ianze na ninyi washiriki. Viongozi wanatakiwa kulibeba hili kwa sababu wanaonekana hawajali sana katika kulisukuma jambo
hili lakini linatakiwa lianze na ninyi”
Mkapa amesema rasilimali zote zinazopatikana katika Bara la Afrika ni za Waafrika na kwamba hiyo ndio hatua ya awali ya kujinufaisha na rasilimali hizo badala ya wengine waliolitawala bara hili ambao wananufaika nazo.
Akiwasilisha mapendezo yaliyotolewa kwenye majadiliano ya siku mbili ya jukwaa hilo, Profesa Andrew Temu amesema Marais wa Afrika wanataka suala la kuhifadhi mazingira na kulinda rasilimali za nchi ziingizwe katika mitaala ya elimu ili kufundisha vijana umuhimu na matumizi yake kwa maendeleo ya Taifa.
Hata hivyo, Rais Magufuli aliwaeleza washiriki Marais Waastaafu kuwa kwa bahati nzuri Serikali ya Tanzania Chini ya uongozi wa Awamu ya Tano, imechukua hatua ya kulinda maliasili zetu ili kusimamia matumizi bora ya maliasili ili tufike mageuzi ya kijamii na kiuchumi.
Kwanza tumetunga sheria ya kulinda Utajiri na Rasilimali zetu za Asili ya mwaka 2017 yaani The Natural Wealth and Resources Permanent Seventy Act of 2017, tumepitia upya na kurekebisha mikataba ya uchimbaji ya madini isiyo na manufaa kwa Taifa., tumeweka msukumo mkubwa katika Ujenzi wa viwanda na ukuzaji wa
tekinolojia ya viwanda ili mazao yanayotokana na maliasili yetu yasindikwe kwanza na kuongeza thamani kabla ya kuuzwa.
Lingine ni kuthibiti uharibifu wa maliasili ya misitu na kulinda bionuai kwa ujumla tunatekeleza miradi mbalimbali ya nishati kama mradi wa bwawa la Nyerere utakao zalisha megawatt 2115 kwenye bonde la mto Rufiji hii kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na kulinda mazingira yetu .
Tanzania imeongeza maeneo ya uhifadhi kwa kuanzisha hifadhi za 3 mpya za Taifa katika ukanda wa Kaskazini Magharibi na ya nne ipo mbioni kuanzishwa kwenye ukanda wa Kusini. Aidha tumechukua hatua nyingine nyingi ikiwemo kudhibiti nidhamu ya utumishi wa umma, ufisadi, rushwa na ubadhilifu tunaamini kwamba
hatua zote hizi zitachangia kwenye matumizi bora ya rasilimali zetu na hatimaye kuleta mageuzi ya kijamii na kiuchumi na kwa bahati nzuri tumeshaanza kuona matokeo ya hatua hizi. Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alimalizia kwa kuwapongeza na kuakisi matokeo ya Mkutano huo kwa kusema kuwa, kwa kuandaa majukwa kama haya kwa ajili ya kubadilishana changamoto za uongozi Barani Afrika. Ni matumaini yangu kwamba majukwaa haya yatakuwa chachu ya mapinduzi ya kifikra na dira miongoni mwa viongozi wa
Afrika na hatimaye kulikomboa bara letu kiuchumi