Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (wanne kulia), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Fortunatus Musilimu(watano kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Kamishna Msaidizi Jumanne Muliro(wapili kulia) wakiwaongoza mabalozi wa usalama barabarani na wananchi wakati wa maandamano ya amani lengo ikiwa kuhamasisha masuala ya usalama barabarrani ili kuepusha ajali za barabarani,maandamano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msadizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza
Mwenywekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza,Ferdinand Chacha, akimwaga chenga maalumu ambazo huonyesha sehemu ya kivuko nyakati za usiku, katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini jijini Mwanza wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza
Mabalozi wa Usalama Barabarani wakiwa katika maandamano ya amani yenye lengo la kuhamasisha Usalama wa Barabarani wakati wakuhadhimisha siku ya mabalozi hao iliyofanyika leo jijini Mwanza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi