NJOMBE
Shule ya sekondari Mlowa iliyokuwa ikibakiliwa na changamoto kubwa ya mikasa ya mimba,utoro na ufaulu duni na kusababisha ya kukosekana kwa nyumba za walimu,mabweni pamoja na miundombinu isiyorafiki ya kutolea elimu kwa wanafunzi imeanza kuona mwanga mara baada mfuko wa kunusuru kaya masikini Tanzania TASAF kwa kushirikiana na wakazi wa kata ya mlowa halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe kuchangishana na kufanikisha ujenzi wa Nyumba nne za walimu,Bweni na Jengo la utawala lenye samani zenye uliogharimu kiasi mil 321 ambapo katika kiasi hicho wananchi wakichangia asilimia 10 ya fedha.
Takribani wanafunzi 8 wameshindwa kuendelea na masomo tangu mwaka juzi baada ya kupata mimba shuleni hapo huku walimu wengi wakitamani kuhama kutokana na kutembea umbali mrefu kutoka vijiji walivyopanga hali ambayo imekuwa na athari kubwa kitaaluma na usalama wa wanafunzi na watumishi.
Baada ya changamoto hizo kubainiwa na waratibu wa TASAF wanalazimika kuweka mkakati wa pamoja na wakazi wa kata ya mlowa ili kuinusuru taaluma shuleni hapo kwa kuhamasishana kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha ujenzi huo jamba ambalo limefanikiwa na kurejesha furaha kwa walimu na wanafunzi kama ambavyo inaelezwa Skontina Matandala ambaye ni mwanafunzi na Rehema Tindwa ambaye ni mwalimu.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi nyumba hizo za walimu, bweni pamoja na jengo la utawala ambazo zimegharimu zaidi ya mil 300 hadi kukamilika kwake Kaimu mkurugenzi wa TASAF makao makuu Christopher sanga amesema kumalika kwa majengo hayo na kuanza kutumika kukawe chachu ya kukua kwa kiwango cha taaluma huku pia akitoa rai kutunzwa na kubuniwa kwa miradi mingine ili kuboresha zaidi miundombinu ya elimu shuleni hapo.
Nae mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema licha ya kuwepo kwa changamoto za miundombinu ya taaluma lakini haridhishwi na mwenendo wa ufaulu shuleni hapo na kutaka uongozi wa shule hiyo kuweka mkakati wa kuinua ufaulu ambao utakuwa na matokeo chanya mpaka kimkoa huku akidai ataendelea kuifatilia kwa karibu shule hiyo.
Nao baadhi ya wananchi akiwemo Emmanuel Odilo wanasema uwepo wa mabweni utasaidia kuinua ufaulu na usalama kwa wanafunzi kwa awali watoto wao walikuwa wakiwindwa na wanaume pindi wawapo njiani kwenda shule .