Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika ufunguzi wa Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James akitoa salamu zake kwa Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi wa Gatsby Africa, Samweli Kilua akitoa taarifa ya namna shirika hilo lilivyoshiriki katika uaandaaji wa Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, kwenye mkutano wa kuboresha mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wwa Mataifa(UNDP), Amon Manyama akichangia hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akiwasilisha mkakati wa maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa Wawakilishi wa Wakurugenzi na wamiliki wa Viwanda vya Kuchambua pamba kutoka kiwanda cha Alliance Ginneries Ltd, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
…………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
Akifungua Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.
“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu, maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika kuyaongezea thamani mazao hayo.
Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini; ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine zaidi ya kuchambua pamba.
Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru
“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora” alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo cha pamba.
Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa kwa vitendo na akazitaka Taasisi za fedha, viongozi na wataalam wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.
Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika.