MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Chongoleani Kata ta Chongoleani Tarafa ya Chumbageni Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kata kwa kata kusikiliza kero zinazowakabili wananchi
MKUU wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Diwani wa Kata ya Mabokweni Jijini Tanga Njama akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akimsikiliza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati wa ziara yake
Sehemu ya wananchi wa Mtaa wa Chongoleani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
SERIKALI mkoani Tanga imewahakikishia wananchi wanaoishi eneo la Chongoleani Jijini Tanga kunapojengwa mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta kutoka hoima nchini Uganda mpaka eneo hilo kwamba itahakikisha wanapata fidia wanayostahili kwa mujibu wa sheria
Huku akiwatoa hofu wananchi hao kwamba wawekezaji wengine ambao watafika kwa ajili ya kuwekeza kwenye maeneo hayo itahakikisha hakutakuwa na vikwazo vya aina yoyote kwenye utoaji wa fidia.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara yake ya Kata kwa Kata iliyoanzia kwenye Kata ya Chongoleani ambapo pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hao.
Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka wananchi hao kuacha tabia ya kuuza ardhi yote walionayo kwa sasa kwani wakumbuke inaweza kuwasaidia kwa ajili ya vizazi vyao vijavyo.
Alisema kwamba hawategemei kuona wananchi wa eneo la Chongoleani wakizulumiwa haki yao kwa misingi ya fidia na baadhi ya watu wanaotaka kupindisha sheria,
“Niwaambie kwamba kila mtu atapata fidia kwa mujibu wa sheria lakini nisema tu tutakuwa na wageni wengi ambao watakuja kwenye shughuli za mradi lazima tujipange vizuri ili isifike mahala tukakosa eneo la kujenga makazi yetu”Alisema
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo wa Mkuu huyo wa mkoa, mtathimini wa Jiji la Tanga Victor Urassa alimueleza mkuu huyo wa mkoa kwamba fidia iliyolipwa imelipwa kwa mujibu wa sheria na kwa usimamizi wa Halmashauri ya Jiji hilo.
Urrasa pia aliwafafanulia wananchi hao kwamba wawekezaji wanapokwenda kwa Mkurugenzi wa Jiji kwa ajili ya kupatiwa ardhi hawajafanya udalali bali wanakwenda huko ili halmashauri iweze kuwasaidia.
Akizungumza mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Chongoleani Zuberi Waziei alisema pia kwamba wawekezaji wanapokwenda maeneo hayo wasipitia sehemu nyengine badala yake wafika kwa wananchi wenyewe ili waweze kuongea nao
“Kwa kweli wawekezaji wakija kuchukua maeneo yetu malipo ya fidia yaongezeke haiwezekani malipo ya Arusha na Tanga yawe tofauti leo ekeri moja ni milioni 2 jambo hilo ni uonevu mkubwa wakae kikao chao waone namna ya kurekebisha suala hili “Alisema mkazi huyo.
Naye kwa upande wake mkazi mwengine Daudi Rafael alieleza kwamba fidia imekuwa ni ndogo hawakufaidika kitu walichopewa wamenua kiwanja wamejenga na hatimaye hata cha kukidhi familia hakuna kitu chochoe.
Alisema mashamba yao yamechukuliwa ni sawa hawakatai ni suala la kimaendeleo lakini mengine yanachukuliwa wanahitaji gharama ziweze kuongezeka wanachohitaji ni kuongezwe fidia.