Naibu waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akiongea na
wananchi wa kijiji cha Tambuu katika wilaya ya Morogoro vijijini
mkoani Morogoro alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ambapo
amezindua rasmi mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko
wa pili.
**************
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
Naibu waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amezindua rasmi mradi wa
umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili katika kijiji cha
Tambuu wilaya ya Morogoro vijijini mkoani Morogoro.
Katiaka uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Tambuu Naibu Waziri
Mgalu amesema kuwa mradi huo utaendelea kuwaungaisha wanachi
hatua kwa hatua katika mambo ya maendeleo na kufungua fulsa za
uchumi kwa wanatambuu.
Kitika ziara yake Mhe. Mgalu ameishukuru Taneco na Rea mkoa wa
Morogoro kwa kazi kubwa walioifanya ya kuhakikisha kijiji cha tambuu
kinaingia kwenye mardi wa Rea ili wananchi waweze kunufaika na
mradi huo unaoendelea katika wilaya hiyo.
Pamoja na kumshukuru Meneja wa Tanesco mkoa wa Morogoro Mhe
Mgalu ameitaka Tanesco kuendelea kuunganisha umeme vijijini bila
kuwalipisha nguzo pamoja na kujipanga kuwahudumia wananchi
kuwaunganishia umeme kwa bei sh elfu 27 tu.
Hata hivyo Mhe Mgalu amtoa wito kwa watanzania watakao pitiwa na
miundominu ya REA kuitunza na kutumia vizuri umeme huo kwa
manufaa yao na taifa kwa ujumla kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo
vitakavyowainua kiuchumi.
Naibu waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amemaliza ziara yake
Mkoani Morogoro ambapo alitembelea mradi wa REA wilaya ya kilosa
na kumalizia walaya ya morogoro vijijini ambapao amezindua rasmi
mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili.