Home Michezo MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DUNIA ATAZIKWA KESHO...

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DUNIA ATAZIKWA KESHO KISUTU

0

Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Ramadhani Nassib (kushoto) amefariki dunia alfajiri ya leo hospital ya Muhimbili

……………..

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ramadhani Nassib amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospital ya Muhimbili mjini Dar es Salaam.
Msiba huo umepkewa kwa majonzi makubwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini, akiwemo Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia, mwili wa marehemu utahifadhiliwa kesho baada ya Sala ya ijumaa katika makaburi ya Kisutu baada ya kusaliwa msikiti wa Maamur, Upanga mjini Dar es Salaam. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.