Home Michezo YANGA KICHWA CHINI YACHAPWA 1-0 NA RUVU SHOOTING MCHEZO WA LIGI KUU...

YANGA KICHWA CHINI YACHAPWA 1-0 NA RUVU SHOOTING MCHEZO WA LIGI KUU VODACOM

0

Mara ya mwisho kufungwa Yanga na timu kutoka Mikoani ni mwaka 2011 ilipofungwa na Mtibwa Sugar hatimaye leo Ruvu Shooting wamevunja mwiko kwa kuichapa bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Vodacom ulionmalizika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaa.

Bao pekee na Ruvu Shooting limewekwa kimiani na Sadat Mohammed akimvisha kanzu kipa Farouk Shikalo mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza.

Bao hilo limeweza kudumu kwa dakika zote 90 mpaka Mwamuzi Martin Saanya alipohitimisha mchezo wa kupuliza kipyenga cha mwisho, ubao ukisomeka 1-0.

Katika mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera aliwatoa wachezaji Sadney Urikhob na kumwingiza Maybin Kalengo, Juma Balinya akimtoa pia na nafasi yake akichukua Balama Mapinduzi lakini mabadiliko hayakuleta mafanikio.

Ruvu imeweka rekodi kwa mara ya kwanza kufuta uteja kwa Yanga tena ikiibuka mshindi ikiwa ugenini.

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia kuanza kesho kwa bingwa Mtetezi Simba kushuka dimbani kucheza na Tanzania Polisi katika uwanja wa Uhuru