******************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametimiza ahadi aliyoitoa ya kugharamia matibabu ya Mgonjwa Ashirafu Hamza aliekuwa akisumbukiwa na tatizo la Saratani iliyopelekea uvimbe kwenye upande mmoja wa uso ambapo tayari mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji mkubwa hivi karibuni na sasa Afya yake imeimarika kwa kiasi kikubwa tofauti na alivyokuwa.
RC Makonda aliona taarifa za Mgonjwa Ashirafu akiomba kusaidiwa matibabu kupitia kituo cha utangazaji cha Clouds Media akiwa Bukoba Mkoani Kagera jambo lililomgusa na kama ilivyo kawaida yake ya kusaidia wenye uhitaji alifanya utaratibu wa kumkatia tiketi ya Ndege ili awahishwe Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya Matibabu na July 27 alitua Uwanja wa Ndege na kuwahishwa Muhimbili.
RC Makonda amesema anamshukuru Mungu kuona hali ya Ashirafu kwa sasa inaendelea vizuri tofauti na alivyoletwa ambapo ametoa wito kwa wananchi kuwa na moyo wa upendo kwa kusaidia watu wenye uhitaji.
Kwa upande Mgonjwa Ashirafu Hamza amesema ameishi kwa tabu na mateso kwa muda mrefu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu lakini anamshukuru RC Makonda kwa kusimama nae bega kwa bega hadi sasa ambapo hali yake kiafya imeimarika baada ya kufanyiwa upasuaji na anajiona amepona.
HUU NDIO UONGOZI UNAOACHA ALAMA.