Mtaalamu wa uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Hamisi Nikuli akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakati wa kikao na wadau wa uvuvi katika Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwenye kikao cha mradi wa Ufuatiliaji wa Asidi Baharini katika Pwani ya Tanzania.
Mtafiti Mkuu wa mradi wa Ufuatiliaji wa Asidi Baharini katika Pwani ya Tanzania kutoka TAFIRI Dkt. Ismael Kimirei (kulia) akitoa maelezo kwa mtaalamu wa uvuvi Dkt. Hamisi Nikuli (katikati) aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAFIRI Dkt. Semvua Mzighani (kushoto) namna boya litakalowekwa baharini karibu na Kisiwa cha Mbudya litakavyokuwa likikusanya taarifa mbalimbali ikiwemo ya wingi wa asidi baharini.
Boya litakalowekwa baharini karibu na Kisiwa cha Mbudya ambalo litakuwa likikusanya taarifa mbalimbali ikiwemo ya wingi wa asidi baharini
Baadhi ya wadau wa uvuvi waliohudhuria kikao cha mradi wa Ufuatiliaji wa Asidi baharini katika Pwani ya Tanzania kilichofanyika katika Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kujadili namna ya kuondokana na wingi wa asidi iliyopo baharini inayosababishwa na ongezeko la hewa ya ukaa.