Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameongoza mazishi ya kaka wa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) Abel Bulugu Kaheza (52) aliyefariki dunia siku ya Alhamis Agosti 22,2019 jijini Dar es salaam akisumbuliwa na kansa ya koo.
Mazishi hayo yamefanyika leo Jumatatu Agosti 26,2019 katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo mamia ya waombolezaji wameshiriki mazishi hayo.
Akitoa salamu za pole na rambirambi,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack amesema :
“Kwa niaba ya serikali na wakuu wote wa wilaya wapo hapa,Mhe.Azza tunakupa pole sana,viongozi wote wa serikali wapo hapa kwa ajili ya kukuunga mkono na kukupa pole kwa msiba huu mkubwa,tunajua wote tumeguswa lakini hatuna namna,tungekuwa na uwezo tungeweza kusema aendelee kubaki lakini kwa kuwa hatuna uwezo tumwachie Mungu”,amesema Telack.
“Namuomba mwenyezi Mungu awape subira katika wakati huu mgumu lakini kikubwa tuendelee kumwombea marehemu kwa mwenyezi Mungu. Siku zote tunasema,msiba uunganishe watu,lakini msiba usichonganishe familia”,ameongeza Telack.
Mhubiri katika ibada ya mazishi alikuwa Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga huku kiongozi wa ibada akiwa ni Nuhu Manoni kutoka kanisa la AICT Tinde.
Abel Bulugu Kaheza alizaliwa Julai 1,1967 na amefariki dunia Agosti 22,2019 wakati akiendelea kupatiwa matibabu ya kansa ya koo katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam.
ANGALIA PICHA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akimpa pole Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza leo nyumbani kwake kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) aliyefiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akimpa pole Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa akimpa pole kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Mbunge wa jimbo la Msalala,Mhe Ezekiel akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa msiba wa Abel Bulugu Kaheza.
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga wakiwa katika msiba wa Abel Bulugu Kaheza leo nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Jeneza lililobeba Mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza likitolewa ndani kwa ajili ya ibada na waombozaji kuaga mwili huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack na wakuu wa wilaya wakiwa wamesimama wakati mwili wa marehemu Abel Bulugu ukitolewa ndani na kuwekwa nje kwa ajili ya ibada na waombolezaji kuuaga.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko,wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiendesha ibada ya mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad leo katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiongoza ibada ya mazishi ya Abel Bulugu Kaheza (ambaye ni kaka wa Mbunge Azza Hilal) leo nyumbani kwa Mbunge Azza Hilal Hamad katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kiongozi wa ibada ya mazishi ya Abel Kaheza, Nuhu Manoni kutoka kanisa la AICT Tinde akizungumza wakati wa ibada ya mazishi nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad leo katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (mwenye kiremba cheusi katikati) akiwa kwenye ibada ya mazishi ya kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Ndugu wa marehemu Abel Bulugu Kahiza wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akitoa salamu za pole na rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akitoa salamu za pole na rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mbunge wa jimbo la Msalala,Mhe Ezekiel akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wabunge 9 wa mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack( watatu kutoka kushoto akiwa msibani. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko,wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiaga mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiaga mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza
Mazishi ya mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza yakiendelea leo Tinde.
Ibada wakati wa mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza ikiendelea.
Ndugu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza
Ndugu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza
Ndugu wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Abdalah Simba na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack.
Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Salum akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ngasa Mboje wakiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog