Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega akiongea na Wavuvi katika Mnada wa Samaki Kunduchi jijini Dar es Salaam baada ya kusikiliza kero zinazowakabili wavuvi hao.
Wavuvi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega baada ya kutembelea mnada wa huuzaji Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega akiongea na wakina mama waliofika katika eneo la Mnada wa uuzaji wa Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akiongea na wavuvi pamoja na wachuuzi wa samaki katika eneo la Mnada wa huuzaji wa samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
***********
NA EMMANUEL MBATILO
Uvuvi haramu wa kutumia mabomu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na takwimu kuonesha ndani ya mwaka huu hakuna tukio lolote lililojitokeza la uvuvi wa kutumia mabomu.
Ameyasema hayo leo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Abdallah Ulega baada ya kutembelea Mnada wa uuzaji Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam na kuwapatia fursa wavuvi wa eneo hilo kueleza changamoto wanazokumbana nazo.
Akizungumza katika mnada huo Mh.Ulega amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Serikali na wavuvi ndo chanzo cha kutokomeza uvuvi wa kutumia mabomu hapa nchini.
“Hakuna mlipuko wa mabomu kwasasa hivyo tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kuna watu wamebaki vilema kwaajili ya hayo mabomu, ninyi mnatakiwa mtuunge mkono kuhakikisha msirudi nyuma, serikali ya awamu ya tano ipo kwaajili ya kushirikiana na wananchi wake”. Amesema Mh.Ulega.
Pamoja na hayo Mh.Ulega amewataka wavuvi kuwa walinzi kati yao na kuhakikisha kila mmoja anafuata utaratibu na sheria zilizowekwa ili kuondokana na usumbufu.
Aidha, Mh.Ulega amesema kuwa suala la wavuvi kutumia Ringnet kuvua samaki aina ya dagaa,Wizara bado inachukua maoni na kuliangalia ninamna gani linaweza kuendelea pasipo kuathiri mazingira pamoja na mvuvi mwenyewe.
Aidha Mh.Ulega amewatoa wasiwasi kuhusiana ukataji holela wa leseni hasa kutemea sehemu ya ukataji na kuwaambia Mheshimiwa Rais ameshaifuta hivyo wanaruhusiwa kutumia leseni hiyo waliyoikata kwa wakati kuitumia katika uvuvi sehe mbalimbali hapa nchini hivyo amewata kufuata utaratibu na sheria katika uvuvi.
“Leseni ya uvuvi ni moja ukikata Mkulanga utatamba nayo mpaka Mtwara, ukikata Mtwara utatamba nayo mpaka Lindi mpaka Tanga”.Amesema Mh.Ulega.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo amewaahidi wavuvi wa eneo hilo kushughulikia suala la ujenzi wa choo ambao utakamilika kufikia mwezi Desemba mwaka kuu mpaka kumalizika ujenzi huo.