Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akiongea na wavuvi pamoja na wachuuzi wa samaki katika eneo la Mnada wa huuzaji wa samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega akiongea na wakina mama waliofika katika eneo la Mnada wa huuzaji wa Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Wavuvi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi, Mh.Abdallah Ulega baada ya kutembelea mnada wa huuzaji Samaki Kunduchi Jijini Dar es Salaam
………………….
NA EMMANUEL MBATILO
Amewataka wakina mama wanaojihusisha na uhuzaji wa samaki aina ya dagaa kutokuwa na hofu kutokana na taarifa zinazosambaa za kukatazwa kwa wavuvi wa samaki hao kuvua hasa kwa kutumia Ringnet.
Ameyasema hayo leo baada ya kutembelea mnada wa huuzaji wa samaki uliopo Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuwa fursa Wavuvi hao kueleza changamoto zao ili aweze kuzishughulikia.
Akizungumza na Wavuvi pamoja na wachuuzi wa samaki waliofika eneo hilo, Naibu Waziri wa Uvuvi na Ufugaji, Mh.Abdallah Ulega amewasisitizia wavuvi waendelee kuvua samaki aina ya dagaa kwa kufuata utaratibu na Sheria pasipo kuharibu mazingira.
Aidha, Mh.Ulega amesema kuwa suala la wavuvi kutumia Ring net wakati wa mchana atawaruhusu kuendelea kutumia ili kuweza kuwapata dagaa ambao ni biashara kubwa kwa wavuvi hao pamoja na wakina mama ambao hufika hapo na kununua kwenda kuuza na kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao.
Aidha Mh.Ulega amewatoa wasiwasi kuhusiuana ukataji holela wa leseni hasa kutemea sehemu ya ukataji na kuwaambia Mheshimiwa Rais ameshaifuta hivyo wanaruhusiwa kutumia leseni hiyo waliyoikata kwa wakati kuitumia katika uvuvi sehe mbalimbali hapa nchini hivyo amewata kufuata utaratibu na sheria katika uvuvi.
“Leseni ya uvuvi ni moja ukikata Mkulanga utatamba nayo mpaka Mtwara, ukikata Mtwara utatamba nayo mpaka Lindi mpaka Tanga”.Amesema Mh.Ulega.
Pamoja na hayo amewapongeza wavuvi kuipa ushirikiano serikali kutokomeza uvuvi harama hasa uvuvi wa kutumia mabomu hivyo kufanya uvuvi huo harama kutokomezwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo amewaahidi wavuvi wa eneo hilo kushughulikia suala la ujenzi wa choo ambao utakamilika kufikia mwezi Desemba mwaka kuu mpaka kumalizika ujenzi huo.