Home Mchanganyiko MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2019 ZAPITISHA MIRADI YOTE YA MAENDELEO WILAYANI...

MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2019 ZAPITISHA MIRADI YOTE YA MAENDELEO WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wiyala ya Itigi kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika juzi Kijiji cha Mkiwa kabla ya  kuanza mbio katika wilaya yake na kukagua miradi ya maendeleo.
 Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Darajani yaliyojengwa na Serikali.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally akivuta pazia kuashiria kufungua madarasa katika Shule ya Msingi Darajani.
 Vijana wa Skauti wakiimarisha ulinzi wakati wa kuupokea Mwenge baada ya kuwasili wilayani Ikungi katika Kijiji cha Mkiwa.

 

 Wanawake wa Kijiji cha Issuna  na wabunge  kutoka wilaya ya Ikungi, Elibariki Kingu na Miraji Mtaturu na wakimbiza Mwenge wakiwa wamebeba vyandarua walivyo kabidhiwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Mzee Mkongea Ally wakati akikagua banda la kujikinga na malaria alipotembelea banda lao.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kulia) akiwatanbulisha Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (kushoto) na Mbunge wa Singida Magharibi,  Elibariki Kingu wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika Kijiji cha Issuna.
 Mbunge Kingu akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Issuna.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Issuna wakiupungia kwa matawi ya miti Mwenge wakati ukipita barabarani.
 Mzee maarufu wa wilayani Ikungi, Said Mughwai (78) akizungumzia historia ya wilaya hiyo mbele ya wakimbiza Mwenge Kitaifa.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akikagua Mnara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere unaojengwa katika viwanja vya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo.
 Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakifurahi wakiwa wamekaa kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
  Taswira ya mnara huo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akipanda mti itakapo tengenezwa bustani kuzunguka mnara huo.
 Mwonekano wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi lililofunguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa.
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mbele ya Ukumbi wa Wilaya hiyo wakati wa uzinduzi rasmi.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ally akimkabidhi kadi ya matibabu ya iCHF mwanafunzi, Ruth Allan wa Shule ya Msingi Ikungi Mchanganyiko wakati wa Uzinduzi wa Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida juzi. Wanafunzi 143 walikabidhiwa kadi hizo walizo katiwa na halmashauri hiyo.
 Muonekano wa jengo la mradi wa maji katika Kijiji cha Ighuka.
 Wanafunzi wakiangalia ukaguzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ighuka.
 Wanawake wa Kijiji cha Ighuka wakiangalia ukaguzi wa mradi wa maji uliokuwa ukifanywa na wakimbiza Mwenge Kitaifa.
 Kijana Mohamed Katende aliyekuwa akitumia dawa za kulevya akizungumza mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge mafanikio waliyopata kupitia ujasiriamala baada ya kuacha kutumia dawa za kulevya na wenzake kufuatia elimu waliyoipata kutoka kwa maofisa wa Polisi wa Kituo cha Puma.
 Viongozi na wananchi wakiwa kwenye mkutano Kata ya Puma.
 Mbunge Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi wa Kata ya Puma.
 Mbunge Elibariki Kingu akizungumza na wananchi wa Kata ya Puma.
 Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano baada ya Mwenge kuwasili kukagua mradi wa Kituo cha Afya.
 Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano baada ya Mwenge kuwasili kukagua mradi wa Kituo cha Afya.
 Makada wa CCM wakiserebuka wakati viongozi wa mbio za Mwenge wakikagua mradi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Sepuka.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru kabla ya kutolewa kiapo cha Utii cha Mwenge katika eneo ulipokesha Viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Sepuka.
 Kiapo cha Utii kwa Rais kikisomwa.
 Mbunge Kingu akicheza sanjari wa Wasanii wa Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Mgungila.
 Baadhi ya Viongozi na Watendaji kutoka Manispaa ya Singida Mjini wakipasha wakati wakisubiri kukabidhiwa Mwenge kutoka Wilaya ya Ikungi katika eneo la Ititi mkoani hapa.
 Mkimbiza Mwenge Kitaifa kutoka Mkoa wa Lindi, Makugu Mwanganya akivikwa skafu na vijana wa Skauti wakati wa makabidhiano ya Mwenge katika eneo la Ititi.
 Wanafunzi wa Shule ya Awali ya Malaika Matumaini ya Singida wakionesha umahiri wa kuruka wakati wa makabidhiano ya Mwenge kutoka Wilaya ya Ikungi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kushoto) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Singida Pasacas Muragiri,  baada ya makabidhiano ya Mwenge.
 Taswira ya makabidhiano ya Mwenge eneo la Ititi.
 Makada wa CCM Wilaya ya Ikungi wakiwa pamoja baada ya Mwenge kukabidhiwa Manispaa ya Singida.
Crew nzima ya Wilaya ya Ikungi wakizungumza machache baada ya Mwenge kumaliza mbio zake wilayani humo  na kuukabidhi Manispaa ya Singida katika eneo la Ititi.
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2019 , Mzee Mkongea Ally amepitisha miradi yote ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 1.162 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani 
Singida na kuwapongeza viongozi wa wilaya hiyo.
 
Pongezi hizo alizitoa juzi wakati Mwenge wa Uhuru ulivyofika kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
 
Miradi mitano ya Maendeleo iliyokaguliwa na kuzinduliwa ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Darajani, Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Ighuka, Mnara 
wa Mwenge wa  Kumbukumbi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi ambapo miradi yote hiyo imegharimu kiasi hicho cha fedha.
 
Akizungumza Wilayani hapo Kiongozi huyo amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kufanya kazi kwa uzalendo ili kuwafanya Watanzania waendelee 
kuiamini Serikali yao chini ya Rais Dk John Magufuli.
 
” Niwapongeze sana Wananchi wa Ikungi kwa namna ambavyo mmeendelea kumuamini Rais wetu Dkt. Magufuli, kipekee nikupongeze DC Mpogolo kwa uzalendo wako unaouonesha toka uteuliwe na Mhe Rais kuwa Mkuu wa Wilaya hii, nikuombe uendelee kuwatumikia wananchi wetu kwa kasi hii hii uliyoanza nayo.
 
” Niwaombe pia ndugu zangu wa Ikungi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na muende kuwachagua viongozi ambao ni waadilifu na wenye kuichukia rushwa, msichague viongozi mafisadi, chagueni watu safi watakaoweza kuwatumikia bila kujali itikadi zenu,” alisema Mzee Mkongea.
 
Kwa upande wake DC Mpogolo ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya Serikali kwa uadilifu pamoja na kuwatumikia wananchi hawa ambao walimuamini Rais Dk Magufuli na kumpa kura.
 
DC Mpogolo amesema atahakikisha wananchi wa Ikungi wananufaika na miradi ambayo imezinduliwa ndani ya Wilaya hiyo ili waweze kuona kazi kubwa ambayo Serikali inaifanya 
katika kuwahudumia.
 
” Miradi hii imegharimu Fedha nyingi upo ujenzi wa madarasa mawili ambayo yanaakisi Sera ya Elimu bure inayosimamiwa na Rais wetu kipenzi, mradi wa Maji kama sehemu ya kampeni 
yetu ya kumtua Mama ndoo kichwani, yote hiyo ni katika kuwatumikia nyinyi wananchi wetu na zaidi kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa kwenu mwaka 2015.
 
 Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu  akihutubia wananchi waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru Kata ya Sepuka alisema tangu Rais Dkt. John Magufuli aingie madarakani amefanya mambo makubwa kwa Watanzania wakiwemo wananchi wake wa Singida Magharibi ambapo amepeleka miradi mingi ya maendeleo ndani ya kipindi cha muda mfupi.
 
Alisema wananchi wa Jimbo lake wamenufaika na miradi ya ujenzi wa Kituo kikubwa cha Afya cha Sepuka kilichowekwa jiwe la msingi juzi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mzee 
Mkongea Ally ambacho kinakwenda kumaliza adha iliyokua ikiwasumbua wananchi wa kata hiyo kwa muda mrefu.
 
” Sisi watu wa Singida Magharibi na Wilaya ya Ikungi tuna mengi ya kumshukuru Rais Magufuli kwa namna alivyotukarimu, miradi mikubwa ya Afya ukiachilia mbali Kituo hiki cha Sepuka lakini pia tumeshapokea takribani Milioni 500 kwa ajili ya Kituo kingine cha 
Iyumbu.
 
” Kwenye maji huko ndio usiseme kila Kijiji tumepanga kuhakikisha kinakua na maji ya kutosha lengo likiwa ni kuakisi kwa vitendo Sera ya Rais Magufuli ya kumtua Mama ndoo, 
ndio maana tunaanza ujenzi wa miradi 14 ya maji na tayari tumeshanunua mitambo miwili ya kisasa kwa ajili ya kumaliza changamoto ya maji pia, ” alisema Kingu.
 
Alisema yeye kama Mbunge anaetokana na CCM ni lazima ahakikishe anasimamia Sera ya Elimu bure kwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa na Hostel ambavyo vyote viko mbioni kukamilika.
 
Alisema miradi yote hiyo imeweza kutekelezwa kutokana na namna Rais Magufuli anavyosimamia kwa uadilifu ukusanyaji wa kodi za Watanzania ambazo zimekua zikitumika kwenye miradi ya maendeleo kote nchini.