Mwasilishajiwa wa sehemu 6-8 ya Sheria namba 5 ya mwaka 2018 Fatma Gharib Haji akiwasilisha mada kwa wajumbe waliyofika katika Mkutano wa kujenga uwelewa wa sheria ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja (katikati) ni Ummy Mohamed Rajab Mwasilishaji wa sehemu 4-5 na wa kwanza kushoto Mkuu wa Kitengo cha Muungano ya Makampuni na Udhibiti wa Ushindani (ZFCC). Mmanga Khamis Machano.
Afisa Mwandamizi Ushauri wa Ushindani kutoka Tanzania bar akitoa Maelezo kwa wadau waliyoshiriki katika mkutanowa kujenga uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja katika ghafla iliyofanyika Ukumbi wa Makonyo Pemba.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Mohamed Jafari Jumanne akitoa ufafanuzi wa kujenga uwelewa wa sheria ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja ghafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Makonyo Pemba.
Wakili wa Serikali kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Asia Ibrahim Mo’hd akitoa ushauri kwa wawasilishaji kuwapatia elimu wafanya bishara na wanunuzi katika mkutano wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja katika ukumbiwa wa Makonyo Pemba.
Mohammed Ali Maalim ambaye ni mjumbe aliyeshiriki katika mkutano wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja akitoa ushauri kwa wafanya bishara kujilinada katika kaizi zao ghafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Makonyo Kisiwani Pemba.
Wajumbe mmbalimbali waliyoshiriki katika mafunzo ya mkutano wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji wakichukuwa wakifuwatilia mkutano huouliyofanyika katika ukumbi wa Makonyo Kisiwani Pemba.
Picha na Miza Othman –Maelezo.
………………………
HASINA KHAMIS ,MAELEZO- PEMBA.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji, Mohamed Jafari Jumanne aliwataka wafanya biashara kuwa mabalozi kwa wenzao kwani wafanyabiashara wengi wanakimbilia kuekeza katika nchi ambazo hazina tume ya ushindani ili kuwarahisisha kuingiza bidhaa bandia.
Hivyo aliwataka wafanya biashara hao kujiorodhesha katika Tume ya ushindani ili kuweza kuepuka kuingiza bidha bandia pamoja na matumizi ya nembo zisizo rasmi.
Hayo aliyasema wakati akifungua mafunzo ya kujenga uwelewa wa Sheria ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja ya Sheria nambari 5 ya Mwaka 2018 ,huko katika Ukumbi wa Makonyo Chake Chake Pemba.
“Miongoni wa umuhimu wa sheria hiyo ya nambari 5 kwa wananchi ni kujua haki zao katika biashara pamoja na kuzuia uingizaji ,uzalishaji wa bidhaa bandia ndani na nje ya Nchi”alieleza.
Aidha Mkurungezi huyo alisema Tume inajitahidi kupambana na bidhaa hizo za bandia zinazoingizwa ikiwemo na wale wafanyabiashara ambao wanatumia nembo za Kampuni nyengine kuvutia wateja .
Pia aliwatoa hofu wananchi juu ya Mchele wa Mapembe ambao ndio chakula kikubwa watumiacho Wananchi wa Visiwa hivi kuwa Mchele unapoingizwa katika Nchi ni lazima kupimwa na kuchunguzwa usalama wa mlaji .
Alisema “wito wangu kwa Wafanyabiashara kuhifadhi bidhaa zao katika sehemu salama ili kuepuka uharibifu kwa bidhaa na kuweza kuleta matatizo kwa Wananchi”.
Hata hivyo alisema viko vitengo mbali mbali vya ukaguzi ambavyo vinapita kila sehemu kukagua bidhaa ambazo zimekwisha muda wake pamoja usalama wa watumiaji.
Pia Mkurugenzi hiyo wa Tume ya ushindani ametoa tahadhari pale panapotokea sadaka ama kutolewa vitu bure ,alisema ni vyema vitu hivyo vikachunguzwa kwanza .
“Ninawaomba Wakuu wa Wilaya ,Mikoa ,Masheha na Watu wengine kuwa waangalifu na bidhaa zinazotolewa kama msaada pamoja na kwenda sehemu husika kutoa taarifa ya msaada huo ili kuweza kupimwa na kuchunguza kwa ajili ya maslahi ya wananchi”alisisitiza.
Akiwasilisha Mada ya sheria nambari 5, Fatma Gharib Haji ,alisema sheria hiyo ina lengo mzuri kwa Wananchi na wafanyabiashara ikiwemo kuwalinda na kuondoa changamoto za Wafanyabiashara wa ndani na nje katika Soko la ushindani.
Nae Afisa Mwandamizi ushawishi wa ushindani kutoka Tanzania bara, Alex Mmbaga nchi nyingi za jumuiya ya maendeleo ya kusini wa Afrika SADC zimejikita katiksa suala la ushindani katika biashara zao.
“Hivyo ni vyema wafanyabiashara wa Zanzibar kuitumia tume hiyo kwa kukuza na kulinda biashara zao kwani tume hiyo ina faida nyingi kwao na wananchi”alieleza.
Kwa upande wao washirika katika mafunzo hayo walisema wameyapokea vyema mafunzo hayo na watakuwa mabalozi kwa wenziwao ili kuona Tume ya ushindani wanaiunga mkono kwa maslahi yao na wananchi
Mafunzo hayo yaliwashirikisha Wafanyabiashara ,Wanunuzi ,Wanasheria ,Vyombo vya ulinzi na usalama ikiwa na lengo la kuiweka wazi Sheria nambari 5 ya Mwaka 2018 ya tume ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji.