Viongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania wakiwa pamoja na waigizaji mbalimbali wa hapa nchini wakiendesha kikao na waandishi wa habari juu ya kuanzisha Tamasha la kuibua vipaji Agosti 25 mwaka huu katika ukumbi wa Harbours club uliopo mivenjini jijini Dar es salaam.
*************
NA EMMANUEL MBATILO
CHAMA cha Waigizaji Mkoa wa Temeke wanatarajia kufanya Tamasha la waigizaji na wasanii wanaoishi katika Wilaya huo litakalofanyika Agosti 25 mwaka huu katika ukumbi wa Harbours club uliopo mivenjini jijini Dar es salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji katika Wilaya hiyo, Bw.Fred Sumari maarufu ‘Dile’ alisema lengo ni kuwakusanya waigizaji wote wanaoishi humo ili kufufua nguvu ya sanaa.
Alisema Temeke ndiyo sehemu iliyoibua na kuzalisha watu maarufu katika sekta ya sanaa, utamaduni na michezo.
“Unavyozungumzia sanaa lazima uutaje mkoa wetu, kwani nusu au robo tatu ya waigizaji wanaoishi Dar es Salaam ni wakazi wa Temeke Kwa mfano Mzee Jongo, Gabo Zigamba, Madebe Lidali, Cathy Rupia, Mboto, Ramy Gals, Patricia Hilaly Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokati Mwegelo na wengine wengi”alisema Dile
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na sanaa mbalimbali na wameandaa Filamu ambayo itachezwa na wasanii 1000 wanaoishi Temeke.