RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019,uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 22-8-2019.kulia kwa Rais Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe.Khamis Juma Mwalim.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani na kushoto Mshauri wa Rais Pemba Mhe. Dk. Maua Abeid Daftari(Picha na Ikulu).
WATENDAJI wa Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar , wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 22-8-2019.(Picha na Ikulu).
KATIBU Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar Ndg. Goerg Joseph Kazi , akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, kulia Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar Mhe. Mzee Ali Haji, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
BAADHI ya Watendaji wa Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, wakati ikiwasilishwa katika mkutano huo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Goerg Joseph Kazi katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
KATIBU wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar , ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu).
MWENYEKITI wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari, akichangia wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar . kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019 kulia Mshauri wa Rais Pemba Mhe. Dk. Maua Abeid Daftari na Waziri wa Wizara ya Sheria Katiba Zanzibar Mhe Khamis Juma Mwalim.(Picha na Ikulu),
**************
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein emesema kuwa
dhamira ya Serikali ya kununua Mtambo mpya wa
uchapaji wa magazeti ni kuhakikisha kiwango cha
uchapishaji wa magazeti ya Zanzibar leo kinaongezeka.
Dk. Shein amesema hayo Ikulu mjini Zanzibar, wakati
akipokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa
Wizara Habari, Utalii na Mambo ya Kale kwa kipindi cha
Julai 2018 – Juni 2019.
Amesema hatua ya Shirika la Magazeti ya Serikali
kuchapisha nakala 1,500 katika mtambo ya ZAGPA kwa
siku ni kidogo mno ikilinganishwa na uwezo mkubwa wa
mtambo huo wa kuchapisha nakala 35,000 kwa saa moja.
Alisema kuwepo kwa mtambo huo kunapaswa kwenda
sambamba na kiwango kikubwa cha uchapishaji wa
magazeti ili yaweze kuwafikia wananchi hadi walioko
mjini na vijijini.
Aidha, alisema kuna umuhimu wa kuwa na Mawakala wa
uuzaji na usambazaji wa magazeti Mikoani, watakaokuwa
na jukumu la kupokea magazeti hayo na kuyasambaza
katika shehia mbali mbali na kuwafikia wananchi.
Katika hatua nyengine, Dk. Shein alieleza haja kwa
baadhi ya vyombo vya habari nchini kutumia vyema
lugha ya Kiswahili, katika utangazaji na uandishi wa
habari akibainisha hali halisi kuwa Zanzibar Mjini ndio
kitovu cha lugha fasaha ya Kiswahili.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuuagiza uongozi wa Wizara
hiyo kukutana na wahariri wa vyombo vya habari, kwa
lengo la kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo.
Aidha, aliitaka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar,
kuweka utaratibu mzuri wa kutoa Vibali vya kupiga
picha, na kusisitiza umuhimu wa kufuatwa sheria za
nchi, hasa kwa wageni wanaokuja kufanya shughuli hizo
hapa Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja ya kuendelea kuzitunza
na kuzihifadhi vyema nyaraka za Serikali.
Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi wa Chuo cha
Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma
kuharakisha utekelezaji wa uamuzi wa serikali wa
kuanza maandalizi ya msingi ili kukiwezesha Chuo hicho
kuunganishwa na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
(SUZA).
Akigusia uendeshaji wa shughuli za makumbusho, Dk.
Shein aliitaka Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale,
kuendelea kuishajiisha jamii ya Wazanzibari, ikiwemo
wanafunzi, kutembelea maeneo hayo ili kufahamu
historia ya asili ya Zanzibar.
Aidha, Rais Dk. Shein alisiitiza haja ya kuendeleza
uhusiano na ushirikiano mwema uliopo katika sekta ya
Utalii, kati ya Zanzibar na Indonesia kwa kushirikiana
na Chuo cha Utalii cha Bali cha nchini Indonesia.
Dk. Shein aliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa
kutekeza vyema majukumu ya kazi zake, sambamba na
kuandaa kwa umakini mkubwa tarifa za Utekelezaji wa
mpango kazi.
Nae, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, alisisitiza
umuhimu wa watendaji an wafanyakazi wa Serikali
kufanya kazi kwa uadilifu na kutoa pongezi kwa Wizara
hiyo kwa mafanikio iliyoyapata sambamba na kuwasilisha
vyema mpango kazi wake.
Mapema, Waziri wa Wizara hiyo, Mahamoud Thabit
Kombo alisema katika kipindi cha Julai – Juni
2018/2019 Wizara imefanikiwa kutekeleza miradi mikuu
mitatu, ukiwemo wa ujenzi wa Studio na Ofisi za ZBC
Pemba, kupitia Kampuni ya ujenzi ya Chuo cha Mafunzo
Zanzibar, ambapo awamu ya kwanza ya kazi hiyo
inayohusisha ghorofa ya chini imekamilika.
Alisema awamu ya pili ya ujenzi huo, Mkandarasi
ataendelea na kazi itakayohusisha ujenzi wa ghorofa ya
pili, uwezekaji, upigaji wa palasta pamoja upakaji wa
rangi.
Aidha, alisema katika kipindi hicho, Wizara
ilishughulikia mradi wa kuimarisha maeneo ya kihistoria
ya Fukuchani na Makamandume, mradi ulioogharimu
shilingi Milioni 850.
Alisema Wizara imeweza kulifanyia matenegenzo
makubwa eneo la kihistoria la Fukuchani, ili kurudisha
sura na haiba yake ya awali.
Alisema matengenezo ya eneo la kihistoria la
Mkamandume yanaendeleo, ukilenga kuziimarisha kuta
za asili katika pande tatu za jengo hilo pamoja na
kuvirudisha baadhi ya vivutio vya asili vilivyomo ndani ya
eneo hilo.
Vile vile, alisema katika kipindi hicho Wizara
ilishughulikia mradi wa kuimarisha Utalii kwa wote,
ukihusisha ujenzi wa kituo cha Utalii katika eneo la Kwa
Bihole Bungi, mradi utakaotumia shilingi Bilioni 1.3 hadi
kukamilika kwake.
Alisema hatua ya kwanza ya ujenzi zimeanza chini ya
Mkanadarasi Quality Building Contarctor, na kubainisha
kuwa pale utakapomalizika utaongeza vivutio vya utalii
nchini, kuimarisha utalii wa ndani na kimataifa, pamoja
na kuongeza ajira kwa jamii, hasa vijana.
Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na uongozi wa
Wizara ya Katiba na Sheria na kuipongeza kwa
utekelezaji mwema wa majukumu ya kazi sambamba na
uwasilishaji mzuri wa taarifa ya mpango kazi.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuishauri Wizara hiyo
kuzingatia haja ya kuwa na utaratibu maalum katika
utengenezaji wa sheria mpya, ili kuwepo mustakbali
mwema wakati ssheria hiyo itakapohitaji kufanyiwa
marekebisho au kufutwa kabisa.
Nae, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mpango kazi
kwa kipindi cha Julai 2018 – Juni 2019, Waziri wa
Wizara ya Katiba na Sheria Khamis Juma Mwalimu
alisema pamoja na mambo mengine Wizara imefanikiwa
kuimarisha mfumo wa sheria kwa kufanya mabadiliko ya
utendaji kazi wa mahakama,Ofisi ya DPP, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu, Polisi, Mafunzo na wadau wengine
wa sheria ili kuwajengea uwezo katika utoaji haki.
Alisema katika utekelezaji wa majukumu yake, Wizara
ilikabiliwa na changamoto ya uhaba wa watendaji hasa
baada kuigaiwa kwa iliokuwa Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria
na Utumishi wa Umma na Utawala bora, pamoja na
kuanzishwa kwa Idara mpya ya msaada wa kisheria.
Aidha, alisema katika kulipatia ufumbuzi suala hilo,
Wizara inakusudia kuajiri watendaji kutoka katika Kada
tofauti ili kukidhi mahitaji ya Wizara.