JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU KUMI NA TATU (13) KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA MBALIMBALI YA KIUHALIFU YALIYOTENDEKA KATIKA MAENEO MBALIMBALI MKOANI MWANZA.
TUKIO LA KWANZA
KWAMBA TAREHE 20.08.19 10:00 HRS MTU MMOJA AITWAYE SAMWEL JOHN @ MTUMWA, MIAKA 26, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MIGOMBANI – LUHAMA WILAYANI SENGEREMA ALIUAWA KWA KUSHAMBULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA FIMBO NA MAWE NA KUNDI LA WAHALIFU (WANANCHI) WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKATI ALIPOKUA AMEHIFADHIWA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA BULYAHIRU AKISUBIRI KUPELEKWA KITUO CHA POLISI BAADA YA KUKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MKUNGU MMOJA WA NDIZI.
HATUA HIYO YA MAUAJI ILITOKEA BAADA YA MWENYEKITI WA KIJIJI HICHO KUJARIBU KUWAZUIA WATU HAO AMBAO WALIANZA PIA KUMSHAMBULIA ALIPOWASILIANA NA POLISI ILI WAFIKE KUMCHUKUA NA POLISI WALIPOFIKA WALIANZA KUSHAMBULIWA NA HIVYO KULAZIMIKA KUMUOKA MWENYEKITI HUYO BAADA YA MTUHUMIWA KUWA AMEUAWA.
KATIKA KUMUOKOA MWENYEKITI HUYO ASKARI NO D 9777 SGT JUMA ALIJERUHIWA KWA JIWE KICHWANI, NA MWENYEKITI BENJAMINI KAHITIRA ALIUMIA KWENYE PAJI LA USO NA WATU WAWILI AMBAO NI DORICA MAJINGO ALIJERUHIWA KWA RISASI KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA NA MUSA MANGE ALIJERUHIWA KWENYE GOTI LA KUSHOTO KWA RISASI BAADA YA KUWA WANAWASHAMBULIA ASKARI POLISI KWA MAWE. MAJERUHI WALIPELEKWA HOSPITALI YA WILAYA SENGEREMA KWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 11 KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AIDHA KAZI YA KUWATAFUTA WATU WENGINE AMBAO WAMEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE BADO INAENDELEA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA WANANCHI WENYE TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAACHE TABIA HIYO KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA, KWA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
TUKIO LA PILI
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAFREDRICK S/O CHENGULA, MIAKA 32, MFANYABIASHARA, MNGONI, MKAZI WA MBEZI – DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU (UTAPELI) KUTOKA KWA MFANYABIASHARA/MUWEKEZAJI WA MADINI AITWAYE MOHAMED MUNNOO, MIAKA 35, RAIA WA MAURITIUS AMBAYE, WALIMTAPELI DOLLA ELFU SITINI (US$ 60,000) SAWA NA TSHS 138,000,000/=, FEDHA ZA KITANZANIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.04.109, BAADA YA MFANYABIASHARA HUYO WA MADINI RAIA WA MAURITIUS KUKUTANA NA WATU HAO (MATAPELI ) WALIOJIFANYA NI M,AAFISA WA SERIKALI NA KUMPELEKA KWENYE OFISI MBALIMBALI ZA KUUZA MADINI YA DHAHABU. AIDHA BAADA YA KUPEWA TAARIFA HIZO RAIA HUYO WA MAURITIUS ALIELEKEZWA KUWEKA PESA KWENYE ACCOUNT YA MMOJA WAO KATIKA EQUITY BENKI TAWI LA MWANZA YENYE NAMBA 3007211416820 FAMM AMTL CO.LTD, ILI AWEZE KUPATIWA MADINI YA DHAHABU YENYE UZITO WA KILOGRAMU 7.
HATA HIVYO BAADA YA MATAPELI HAO KUINGIZIWA KIASI HICHO CHA FEDHA WALITOROKA, UFUATILIAJI ULIWEZESHA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI. NA BAADAE KIONGOZI WAO NAE AMEKAMATWA AKITOKEA NCHI JIRANI.
IMETOLEWA NA:-
Muliro J. MULIRO-ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
21 AGOSTI 2019.