Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili  ZUNGU PAULO @ TINYA  [45] na BARAKA LAZARO @ TIMOTHEO [40], wote  wakazi wa Kijiji na Kata ya Lupa  wakiwa na nyara za Serikali vipande vitatu [03] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe  19.08.2019 saa 20:00hrs  katika Kijiji na Kata ya Lupa,  Tarafa ya Kipembawe Wilaya ya Chunya.     Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Mbinu iliyotumika ni kuhifadhi pembe hizo kwenye mfuko wa Sandarusi na kutafuta wateja. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili  IGELELE DANIEL  [42] na NYIRENDA JOHN @ DAIMON  [32], wote  wakazi wa Kijiji cha Isangawana  wakiwa na nyara za Serikali vipande kumi [10] vya meno ya Tembo bila kibali.

Tukio hilo limetokea tarehe  19.08.2019 saa 20:15hrs  katika nyumba ya kulala wageni iitwayo UZUNGUNI chumba namba 113 iliyopo eneo la Sinjilili, Kata ya Itewe, Tarafa Kiwanja, Wilaya ya Chunya.    Thamani ya Nyara hizo bado kufahamika. Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe Mahakamani.

AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA KIFO.

Jeshi la Polisi linamtafuta dereva mmoja ambaye alikimbia baada ya kutokea ajali na kusababisha kifo cha  askari MT. 90399 CPL FRED GRAYSON @ MBALIZI [35] askari wa JWTZ Kikosi cha 44KJ – Mbalizi, mkazi wa Iwambi. 

Tukio hilo limetokea tarehe 20.08.2019 saa 21:15hrs eneo la ZZK – Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini katika baraaaaaabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma. Katika tukio hilo marehemu alikuwa akiendesha gari  ndogo T.219 CSU  Nissan akitokea Songwe Airport kuelekea Mbalizi na kugongana uso kwa uso na gari kubwa T.838 APZ Scania Lori ambalo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kueleka Tunduma hivyo kusababisha kifo chake papo hapo. Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo [marehemu] kujaribu kulipita gari linguine lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari. Jitihada za kumtafuta dereva ambaye alikimbia mara baada ya ajali zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali teule ya Ifisi. 

OPERESHENI DHIDI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni na ukaguzi wa vyombo vya moto katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya vinavyokiuka sheria za usalama barabarani. Hivyo wamiliki wa Bajaji na madereva ni vyema wakafuata na kutii sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika. Zoezi hilo la ukaguzi na ukamataji wa vyombo vya moto kwa makosa mbalimbali ni endelevu katika mkoa wetu. 

WITO:

Natoa wito kwa jamii kutoa taarifa katika mamlaka husika juu ya mtu/watu/kikundi au mtandao unaojihusisha na matukio ya ujangili ili hatua kali za kisheria dhidi yao zichukuliwe.

Imetolewa na :

[ ULRICH O. MATEI – SACP ]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.