Home Mchanganyiko SERIKALI INAUNGA MKONO JITIHADA ZA KUWAPA VIJANA MBINU NA NYENZO ZA KUTAMBUA...

SERIKALI INAUNGA MKONO JITIHADA ZA KUWAPA VIJANA MBINU NA NYENZO ZA KUTAMBUA FURSA NA KUZIFANYIA KAZI-MH.MHAGAMA

0

Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Ajirana Walemavu,Mh.Jenista Mhagama(Mb) akiongea katika uzinduzi wa mafunzo ya wajasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Wajasiriamali walioweza kuhudhulia ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo vya elimu ya juu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

******************

NA EMMANUEL MBATILO

Serikali imeweka taratibu za kuanzisha na kuimarisha vituo vya uatamizi ili biashara changa zinazofunguliwa ziweze kupata uangalizi wa kitaalamu na ziweze kukua kabla ya kuingia katika soko huru na kupambana na ushindani kutoka kwa wazoefu.

Ameyasema hayo leo Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Ajirana Walemavu,Mh.Jenista Mhagama(Mb) katika uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo,Mh.Mhagama amesema kuwa serikali inaunga mkono juhudi hizo kwasababu imekuwa inatambua umuhimu wa vijana kujenga uchumi wa nchi.

Aidha, Mh.Mhagama amesema kuwa ni uamuzi makini na wakijasiri kwa wanataaluma na wenye elimu ya juu kuamua kurudi katika jamii na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali.

“Ni imani yangu kuwa uamuzi haukufanywa kwa bahati mbaya bali mmesoma alama za nyakati na kuamua kuchukua nafasi yenu ndani ya jamii”.Amesema Mh.Mhagama.

Mh.Mhagama amesema kuwa kutokana na miradi mingi ya muhimu inayoendelea hapa nchini hivyo itaibua fursa kwa vijana kujipatia ajira na kujikwamua kimaisha pamoja na kuondokana na janga la ukosefu wa ajira.

Pamoja na hayo Mh.Mhagama amewataka vijana wajitahidi kujitengenezea ajira kwa kujiajili kuliko kusubiri ajira imfuate kwani maisha yamebadilika na wengi wanahitaji ajira.

Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.William Anangisye amesema kuwa wazo la kuandaa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliomaliza masomo katika vyuo vya elimu ya juu Tanzania limetokana na utafiti walioufanya na kugundua kuwa pamoja na kwamba kuna fursa nyingi za ujasiriamali ambazo bado hazijafanyiwa kazi, vijana wengi waliomaliza elimu ya juu wanahangaika kutafuta kazi za kuajiriwa ama na serikali au mashirika binafsi.

“Kama sote tunavyofahamu, siku hizi ajira ni adimu na wakati mwingine huchukua muda mrefu mpaka kupatikana na hivyokuwaathiri vijana wengi.Hivyo tulibaini kuwa jitihada kubwa inahitajika kitaifa kuwawezesha vijana kutambua changamoto za kijamii zilizopo na kujaribu kuzibadili kuwa fursa kwa kubuni ufumbuzi utakaopelekea utengenezaji wa ajira”. Amesema Prof.Anangisye.

Aidha, Prof.Anangisye amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa katika makundi ya vijana wasiozidi 50 kwa darasa kwa muda wa siku tatu mfululizo na yatatolewa bila malipo yoyote.