BAADHI ya Wanachama wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar wakifuatilia hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya yao uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikapidhiwa Cheti cha Shukrani na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Ndg. Masururu Saadun Ferouz, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar , kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Maudline Castico.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Ndg. Masururu Saadun Ferouz akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wanachama wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) wakiitikia dua ikisoma na Mwanachama wa Jumuiya hiyo Sheikh Gharib Bakari Seif kutoka Kijiji cha Gana Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
*******************
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braaza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka jamii
kuzingatia umuhimu wa kuwaheshuimu na kuwatendea
wema wazee, kwa kutambuwa kuwa ni misingi muhimu
ya silka, malezi na utamaduni wa Wazanzibari.
Dk. Shein amesema hayo leo katika ufunguzi wa
mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazee na Wastaafu
Zanzibar (JUWAZA), uliofanyika katika ukumbi wa
Sheikh Idris Abdul wakil, Kikwajuni mjini hapa.
Amesema jamii imekumbwa na vitendo vya udhalilishaji
na unyanyapaa dhidi ya wazee, huku kukiwa na watu
ndani ya familia wanaowadharau wazee wao kwa
kuwatukana pamoja na kuwahusisha na imani za
kuwashirikina na dhana za kuhusika na vitendo viovu,
ikiwemo uchawi na wanga.
Alisema kuna baadhi ha vijana mbali na kusomeshwa
vyema na wazee wao, wamekuwa wakiwadharau wazee
kwa kigezo kuwa hawaendani na hadhi walizonazo,
mambo yanayochangia na kuwafanya wazee kukosa
amani, matunzo, misaada na haki wanazostahiki.
“Haki ya kuheshimiwa na kutunzwa ni ya msingi kwa kila
mzee, vijana wana wajibu wa kuwapa wazee wao haki zao
kwani huo ni wajibu wao”, alisema.
Aliitaka jamii kuendelea kuwaheshimu wazee kutokana
na mambo mbali mbali makubwa waliyolifanyia Taifa na
kusisistiza haja ya kuendelea kuwatunza an kuwaenzi ili
kupata fursa ya kuchota hekima na busara kutoka kwao.
Alisema nchi zote zinazoendelea zimekuwa na utamaduni
wa kuwaenzi na kuwathamni wazee na wastaafu na
kuwatumia ipasavyo, hususan pale kunapohitajika
ushauri wa mambo mbali mbali, kutokana ana maarifa,
hekima na uzoefu wao katika masuala ya kimaisha.
Aidha, alisema ni muhimu kuzingatia suala la kuwatunza
wazee kuwa limetiliwa mkazo katika mafunzo ya Dini
zote, ikiwa ni hatua maalum katika kuwatendea wema.
Dk. Shein alisema katika kudhihirisha dhamira njema ya
Serikali katika kuyashughulikia masuala ya wazee, mara
baada ya Mapinduzi matukufu ya 1964, Rais wa kwanza
wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume alianzisha
ujenzi wa nyumba za wazee kwa lengo la kuwahifadhi,
hususan wale waliokosa uwezo na watu wa kuwahudumia.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa
ikiendeleza utaratibu wa kuwapa hifadhi na
kushughulikia changamoto mbali mbali zinazowakabili
wazee, kwa kutambuwa kuwa huo ni wajibu wake wa
msingi.
“Lazima tuwathamini wazee wetu, tuwaheshimu na
tuwahifadhi kwa kusikiliza shida zao na kuzitafutia
ufumbuzi kwa kadri ya uwezo wetu”, alisema Dk Shein.
Aidha, alibainisha kuwa wajibu wa kuyashughulikia
masuala yanayowahusu waze ni hatua ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa 2015 – 2020, kama
ilivyoainishwa katika Ibara ya 135,
Dk. Shein alieleza taarifa ya Idadi ya watu na
iliofanyiika mwaka 2012 imebainishwa kuwepo zaidi ya
wazee 53, 311 wenye umri wa kuanziza miaka 60, hatua
iliyoifanya Serikali kuanzisha Wizara ya Kazi,
Uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto baada ya
kutambua thamani yao.
Aidha, alisema Serikali ilianzisha Sera ya Hifadhi ya
Jamii mnamo mwaka 2014, kwa lengo la kusimamaia
wazee wote nchini, ikiwemo wenye umri wa kuanzia
miaka 70 na kuendelea na kuwapatia posho la shilingi
20,000 kila mwezi.
“Serikali itaendelea kuyaimarisha makaazi yao na
kuhakikisha kuwa wazee hao wanapewa huduma zote
muhimu wanazostahili, zikiwemo za chakula, matibabu,
maji safi na salama pamoja na ulinzi wa maisha yao”,
alisema.
Dk. Shein aliweka wazi malengo ya serikali ya kuwapatia
wazee hao mazingira bora zaidi ya kuishi ikiwa pamoja
an kuwaandalia ziara za kuzitemebelea sehemu mbali
mbali za kihistoria na za maendeleo.
Alisema amefurahishwa sana mafanikio makubwa
yaliopatikana kupitia JUWAZA kutokana na kazi kubwa
ya kuwaunganissha wazee kwa lengo la kuimarisha hali
zao kiafya, kiuchumi na ustawi bora wa maisha yao.
Akigusia maomba mbali mbali yaliowasilishwa kwake, Dk.
Shein alisema Serikali inalifanyia kazi ombi la kuongeza
kiwango cha posho ya Pensheni jamii na kuahidi
kulitolea uamuzi kutegemea na wakati husika.
Sambamba na hilo, Dk. Shein alisema ni jambo zuri
kuwepo kwa sheria, itakayozingatia mambo mbali mbali
ya wazee, huku akionyesha imani kubwa aliyonayo ya
Rais ajaye kuendelea na ataratibu wa utoaji wa Pensheni
jamii kwa kuzingatia kuwa atakuwa na uelewa mpana wa
Ilani ya CCM.
Aidha, Dk. Shein alikubali kuwa mlezi wa Jumuiya ya
Wazee na Wastaafu (JUWAZA) pamoja na kuunga
mkono rai ya uanzishaji wa mfuko maaalum, ili kusaidia
shughuli mbali mbali za kuendeleza Jumuiya hiyo.
Katika hatau nyengine, Dk. Shein alipokea Cheti cha
Uongozi bora kutoka JUWAZA pamoja kupokea Kadi ya
Uanachama wa Jumuiya hiyo.
Nae, Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Wanawake na watoto Modline Castico, alisema kuwepo
kwa mswada wa sheria kuhusiana na utoaji wa Pensheni
jamii, umewafanya wazee kufurahia jambo hilo, kwa
kuzingatia kuwa utawahakikishia ulinzi wa haki zao,
sambamba na kuondokana na vitendo vya udhalilishaji.
Alisema Wizara hiyo itaendelea na juhudi zake za
kupigania na kuimarisha haki na ustawi bora wa maisha
ya wazee nchini.
Mapema, akisoma Risala ya Jumuiya hiyo, Amour Haji
Nassor aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa
kuongeza kiwango cha Posho la Pensheni jamii kwa
wastani wa asilimia hamsini ya kima cha chini cha
mshahara, kabla ya kumaliza kwa awamu ya saba ya
Uongozi.
Aidha, alipongeza juhudi kubwa zinazochukuliwa na
Serikali katika kuwapatia wazee huduma mbali mbali za
kijamii, ikiwemo suala la afya bora , akibainisha juhudi
hizo zimefanikiwa kuimarisha hali zao.