Na.Alex Sonna,Dodoma
Madereva Daladala zinazofanya kazi katikati ya Jiji la Dodoma leo wamegoma kuendelea na kazi ya kusafirisha abiri, wakishinikiza kuondolewa kwa wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama machinga kuondolewa katika eneo hilo kwani hawafanyi kazi kwa uhuru.
Mgomo huo uliyoanza tangu majira ya asubuhi umesababisha umati mkubwa wa watu kushindwa kuendelea na majukumu yao ya kila siku kwa kukosa usafiri.
Wakizungumza na vyombo vya habari katika standi ya sabasaba Jijini Dodoma mwenyekiti wa waendesha daladala standi ya sabasaba Shukuru Mushi amesema wameamua kugoma kutokana na maombi yao kutofanyiwa kazi ya kuomba machinga kuondolewa kutokana na kujazana na kuleta ugumu wa waendesha daladala.
“Eneo limekuwa dogo tunashindwa kufanya kazi kwa uhuru tukipaki vibaya askari wanatupiga faini, wakati ndani ya standi kumejaa wafanyabiashara, mbaya zaidi kuna wengine wanachoma mishkaki karibu na magari na wengine wanatumia gesi kuchoma samaki hii ni hatari” amesema Mushi.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alifika eneo la tukio na kuwaomba madereva kuendelea na shughuri ya kusafirisha abiria huku juhudi mbalimbali za kutatua kero hizo zikiendelea.
Na amepiga marufuku shughuri mbalimbali ikiwamo kuchoma mahidi na mishkaki katika eneo hilo na kutaka watu hao kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa kwa shughuri.
Pia amebainisha kuwa wapo mbioni kuanzisha stendi nyingine eneo la Makole ili kuondoa msongamano katika stendi hiyo ya sabasaba ikiwa ni stendi kubwa inayotumiwa na wakazi wengi wa Jiji la Dodoma.