Home Biashara KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI AIRTEL INATOA HUDUMA NCHI TANO ZA SADC

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI AIRTEL INATOA HUDUMA NCHI TANO ZA SADC

0

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Bi. Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika nchi tano za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ambazo ni Tanzania, Zambia, Malawi, Madagascar na Shelisheli.

 Amezungumza hayo katika banda la kampuni hiyo lililopo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere Posta  Jijini Dar es salaam ambako Mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC unafanyika.

Beatrice Singano amesema kampuni ya simu ya AIRTEL imejizatiti katika kutoa huduma mbalimbali za mawasiliano zilizobora kabisa  ili kuwarahisisha mawasiliano ya wateja wake wote waliomo katika nchi hizo za Jumuiya ya SADC.