Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Salim Abdulla Salim akichangia kitu katika Mkutano huo wa takwimu za ajali na makosa ya barabarani.
Picha na Makame Mshenga.
…………………
Na Mwashungi Tahir,Maelezo
Elimu inahitajika zaidi kutolewa kwa jamii ili kupunguza ajali za barabarani na kutambua makosa ya barabarani ambayo hujitokeza mara kwa mara na kusababisha athari .
Hayo ameyasema Koplo Ali Abdullah Juma Polisi Trafic kutoka Makao Makuu huko katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makosa ya barabarani .
Amesema lengo la kutolewa elimu hiyo kwa jamii ni kuona ajali zinapungua kila tukienda mbele na hatimae kumalizika kabisa ili kuweza kunusuru ajali zinazoweza kuepukika .
Hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwa na mashirikiano katika kuelimisha jamii ikiwemo madereva, abiria , wanaoendesha baskeli,na wanaotembea kwa miguu.
Akiwasilisha mada ya toleo la Takwimu za Ajali na makosa ya barabarani kwa Zanzibar Julai,2019 Asha Mussa Mahfoudh Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali amesema takwimu za ajali barabarani hutoa taarifa za ajali zinazotokea.
Amesema lengo la kutolewa toleo hilo ni kutoa taarifa za ajali na makosa barabarani za ndani ya Zanzibar ambazo ni muhimu na hutumiwa na wapangaji , watunga sera , na watoa maamuzi.
Pia amesema Jumla ya makosa ya barabarani 1,749 yameripotiwa mwezi Julai, 2019 , ambapo makosa hayo yote yanaongozwa na wanaume hivyo kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.
Aidha amesema Wilaya ya Mjini ina idadi kubwa ya makosa ya barabarani ambapo makosa 401 sawa na asilimia 22.9 kati ya makosa yote yaliyoripotiwa na Wilaya ya Micheweni ina idadi ndogo ya makosa ya barabarani yaliyoripotiwa ni 15 asilimia 0.9.
Hivyo Wilaya ya Mjini , Magharibi ‘A’ na Magharibi ‘B’ zimeongoza zaidi kwa makosa ya kushindwa kuvaa sare na beji kwa utingo na dereva kwa gari za abiria, kutofuata miongozo na kanuni za usalama barabarani.
Vile vile makosa mengine ni pamoja na kuendesha chombo cha moto gari,vespa,pikipikififti bila ya leseni, bima na leseni ya njia, kuendesha chombo ca moto bila kuvaa helment na kuzidisha idadi ya abiria na mizigo.