Home Mchanganyiko KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MATUMIZI YA BAJETI

KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MATUMIZI YA BAJETI

0

Na Omary Machunda – Bunge

Mtaalamu wa Ukaguzi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Ndg. Emmanuel Tutuba ameendesha Semina kuhusu Dhana na Uzoefu wa Usimamizi wa matumizi ya Bajeti nchini Tanzania kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC.

Semina hiyo imefanyika jana kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma ikifadhiriwa na Ofisi ya Bunge kupitia Mradi wa Uwezeshaji wa Wabunge na Watumishi wa  Ofisi hiyo.

Wakichangia mada katika semina hiyo, mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Omary Kigua (Mb) alisema kuna umuhimu kwa vyombo kama vile Takukuru, Tamisemi na Ofisi za Ukaguzi  kushirikiana kwa pamoja ili kuzisaidia mamlaka mbalimbali za umma kuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya bajeti ya Serikali.

Naye mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Juma Omar (Mb) alitaka kujua ni kwa kiwango gani maoni ya wataalamu hao yamekuwa yakifanyiwa kazi kwa maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka alisisitiza umuhimu wa kupewa mafunzo hayo.

 “Mafunzo haya ni muhimu kwa Kamati yetu lakini pia ni muhimu kwa Wabunge wote ili kutuwezesha kujua namna bora ya uzimamizi wa matumizi ya bajeti kwenye miradi inayokuja majimboni mwetu”